• HABARI MPYA

  Thursday, February 15, 2018

  DEUS KASEKE, DIHILE WAFUNGIWA ASFC NA KUPIGWA FAINI KALI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewafungiwa mechi tatu na kuwatoza faini ya Sh. 500,000 kila mmoja wachezaji Deus Kaseke wa Singida United na Shaban Dihile wa Green Warriors kwa makosa ya kinidhamu.
  Katika kikao chake cha Februari 13, mwaka huu, ambacho pamoja na mambo mengine ilipitia taarifa za mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya Green Warriors na Singida United, Kamati imewatia hatiani wawili hao kwa kosa la kutoingia uwanjani na timu zao na hawakuwepo wakati timu hizo zikipeana mikono Januari 31 Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
  Deus Kaseke anaweza kuichezea tena Singida United michuano ya ASFC kama itafuzu fainali tu 

  Taarifa ya Kamati kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya ASFC(1) ambayo inaelekeza kutumika kanuni ya ligi husika na hivyo kanuni iliyotumika ni 37(7d).
  Katika hatua nyingine, mchezaji mwingine wa Singida United Kambale Salita amepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu pinzani kwenye mchezo huo.
  Wakati huo huo: Kikao cha kawaida cha kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kinakutana Jumamosi  Februari 17,2018 kwenye Hoteli ya Sea Scape,Mbezi Beach,Dar Es Salam.
  Kikao hicho cha kawaida kinachokutana kila baada ya miezi mitatu kitakuwa na ajenda kwa mujibu wa katiba ya TFF kupitia na kutathmini utendaji wa Shirikisho.
  Kikao hicho cha kamati ya Utendaji kinatanguliwa na vikao vya kamati mbalimbali za TFF ambazo zimeanza kukutana kwa wiki mbili na wiki hii vikao vya kamati hizo vinaendelea.
  Wajumbe wa Kikao cha kamati ya Utendaji wanaanza kuwasili kesho Ijumaa Februari 16, 2018 na watafikia kwenye Hoteli ya Sea Scape. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DEUS KASEKE, DIHILE WAFUNGIWA ASFC NA KUPIGWA FAINI KALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top