• HABARI MPYA

  Monday, February 12, 2018

  AL MASRY YAWATUMIA UJUMBE SIMBA SC KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

  TIMU ya El Masry imeanza vyema Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza juzi mjini Cairo.
  Masry, inayofundishwa na gwiji wa Misri, Hossam Hassan juzi ilicheza katika Uwanja wake wa nyumbani, Port Said kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano ya kucheza ugenini kufuatia kufungiwa kwa sababu ya vurugu mwaka 2012.
  Ikumbukwe, Masry wakivuka raundi hii watakutana na mshindi wa jumla kati ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnare ya Djibouti.  Simba nayo jana ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
  Mabao ya Masry yalifungwa na Islam Salah dakika ya 14, nyota wawili kutoka Burkina Faso Aristide Bance dakika ya 40 na Mohamed Koffi dakika ya 52 na Islam Issa dakika tisa kabla ya filimbi ya mwisho.
  Masry sasa watasafiri kuwafuata Green Buffaloes kwenda kuulinda ushindi wao huo kwenye mchezo wa marudiano Februari 20.         

  MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO
  Ijumaa Februari 9, 2018
  Djoliba (Mali) vs ELWA United (Liberia)*
  Onze Createurs (Mali) 1-1 CR Belouizdad (Algeria)
  Jumamosi Februari 10, 2018
  Petro Atletico (Angola) 5-0 Masters Security (Malawi)
  Young Buffaloes (Swaziland) 0-1 Cape Town City (Afrika Kusini)
  Costa do Sol (Msumbiji) 1-0 Jwaneng (Botswana)
  Energie (Benin) 1-0 Hafia (Guinea)
  Ngazi Sport (Comoro) 1-1 Port Louis (Mauritius)
  Mangasport (Gabon) 0-1 Maniema Union (DRC)
  Olympic Star (Burundi) 0-0 Etoile Filante (Burkina Faso)
  New Stars (Cameroon) 2-1 Deportivo Niefang (Equatorial Guinea)
  Tanda (Ivory Coast) 0-0 CS la Mancha (Kongo)
  Al Ittihad (Libya) 1-0 Sahel (Niger)                                    
  El Masry (Misri) 4-0 Green Buffaloes (Zambia)
  US Ben Guerdane (Tunisia) vs Hilal Juba (Sudan Kusini)**
  Jumapili February 11, 2018
  APR (Rwanda) 4-0 Anse Reunion (Shelisheli)
  Akwa United (Nigeria) 1-2 Hawks (Gambia)
  Asante Kotoko (Ghana) 1-0 CARA (Kongo)
  AFC Leopards (Kenya) 1-1 FOSA Juniors (Madagascar)
  Simba (Tanzania) 4-0 Gendarmerie (Djibouti)
  RS Berkane (Morocco) 2-1 Mbour Petite Cote (Senegal)
  Africa Sports (Ivory Coast) 1-1 FC Nouadhibou (Mauritania)
  Zimamoto (Zanzibar) 1-1 Wolaitta Dicha (Ethiopia)
  *ELWA United imejitoa na US Ben Guerdane imepewa ushindi wa 3-0 baada ya Hilal Juba ya Sudan Kusini kutotokea uwanjani
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL MASRY YAWATUMIA UJUMBE SIMBA SC KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top