• HABARI MPYA

  Monday, February 12, 2018

  AS VITA YAIFUMUA 4-0 WANDERERS LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  VIGOGO wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Vita wameanza vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afriuka baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Be Forward Wanderers katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Uwanja wa Matyrs mjini Kinshasa jana.
  Wakitumia mfumo wa kujihami wa 4-5-1 huku wakicheza na mshambuliaji mmoja tu Peter Wadabwa, Wanderers waliwapa wakati mgumu wenyeji mwanzoni mwa mchezo.
  Lakini mambo yakabadilika dakika ya 17 baada ya Ducapel Moloko kufunga bao la kwanza akimtungua kipa wa Wanderers, Richard Chipuwa.
  Wenyeji wakaongeza mabao matatu kupitia kwa Mukoko Batezadio dakika ya 29 na Jean-Marc Makusu Mundele dakika tatu kabla ya mapumziko. Moloko akafunga na la nne dakika ya 87.
  Kocha wa AS Vita, Florent Ibenge alifurahishwa na matokeo hayo, wakati mpinzani wake, Yasin Osman, alisema kwamba timu yake ianakabiliwa na mtihani wa kuupanda mlima mrefu katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Taifa wa Bingu mjini Lilongwe, Jumatano ya Februari 21, 2018.
  Township Rollers ikatumia vizuri fursa ya kucheza nyumbani, Botswana kwa kuwachapa 3-0 El Merreikh ya Sudan. Ikumbukwe mshindi kati ya Township Rollers na El Merreikh atakutana na mshindi kati ya Yanga ya Tanzania na Saint Louis Suns United ya Shelisheli.

  MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA KWANZA LIGI YA MABINGWA
  Jumamosi Februari 10,  2018
  CNaPs Sport (Madagascar) 2-1 KCCA (Uganda)
  Zanaco (Zambia) 3-0 Armed Forces (Gambia)
  Stade Malien (Mali) 1-1 Williamsville AC (Ivory Coast)
  RC Kadiogo (Burkina Faso) 1-0 Mounana (Gabon)
  AS FAN (Niger) 1-3 Horoya (Guinea)
  Generation Foot (Senegal) 2-0 Makkassa (Misri)
  Yang Africans (Tanzania) 1-0 Saint Louis (Shelisheli)
  Township Rollers (Botswana) 3-0 El Merreikh (Sudan)
  Gor Mahia (Kenya) 2-0 Leones Vegatarianos (Equatorial Guinea)
  Concorde (Mauritania) 1-1 Esperance (Tunisia)
  AC Leopards (Kongo) 2-1 AS Port (Togo)
  JKU (Zanzibar) 0-0 Zesco (Zambia
  Difaa El Jadida (Morocco) 10-0 Benfica (Guinea Bissau)
  Bidvest (Afrika Kusini) 2-0 Pamplemousses (Mauritius)
  Rayon Sports (Rwanda) 1-1 Lydia Academic (Burundi)
  Jumapili Februari 11, 2018
  Saint George (Ethiopia) vs Al Salam Wau (Sudan Kusini)
  Bantu (Lesotho) 2-4 Mbabane Swallows (Swaziland)
  El Tahadi (Libya) 1-0 Aduana (Ghana)
  ES Setif (Algeria) 6-0 Olympic de Bangui (CAR)
  AS Real (Mali) 1-1 MFM (Nigeria)
  AS Otoho (Kongo) 2-0 MC Alger (Algeria)
  Plateau United (Nigeria) 3-0 Eding Sport (Cameroon)
  LISCR (Liberia) 1-0 El Hilal (Sudan)
  Buffles (Benin) 1-1 ASEC Mimosas (Ivory Coast)
  Ngaya (Comoro) 1-1 UD Songo (Msumbiji)
  AS Vita (DRC) 4-0 Be Forward (Malawi)
  Primeiro de Agosto (Angola) 3-0 FC Platinum (Zimbabwe)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AS VITA YAIFUMUA 4-0 WANDERERS LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top