• HABARI MPYA

  Thursday, January 18, 2018

  YANGA YASEMA LWANDAMINA ATAPATA KIBALI KIPYA LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imesema kwamba kocha George Lwandamina atapatiwa kibali kipya cha kufanya kaiz nchini leo kufuatia cha awali kumaliza muda wake.
  Kwa mara ya pili mfululizo, Mzambia Lwandamina jana alikuwa jukwaani wakati timu yake ikicheza na Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kama ilivyokuwa wiki iliyopita katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA.
  Lwandamina alikuwa jukwaani Uwanja wa Amaan, Zanzibar Yanga ikitolewa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 ingawa alikuwa ana siku mbili tangu arejee kutoka kwao Zambia kwa matatizo ya kifamilia.
  George Lwandamina (kushoto) akiwa jukwaani jana Yanga ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu 

  Na jana, Lwandamina alikuwa jukwaani akiishuhudia Yanga ikilazimishwa sare ya 0-0 na Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru.
  Ofisa Habari wa Yanga, Dissmas Ten ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba suala la kumpatia Lwandamina kibali kipya litakamilika leo ili aendelee na kazi Jangwani.   
  Lwandamina alikuwa kwao, Zambia tangu Desemba mwaka jana, kwanza kuhudhuria hafla ya mwanaye wa kike kuhitimu masomo ya chuo, na akiwa huko ukatokea msiba wa mwanawe wa kiume uliomfanya akae kwa muda mrefu kabla ya kurejea nchini wiki iliyopita.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASEMA LWANDAMINA ATAPATA KIBALI KIPYA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top