• HABARI MPYA

  Friday, May 05, 2017

  MOURINHO KUWAPUMZISHA NYOTA WAKE MECHI NA ARSENAL

  Marcus Rashford akiwa huku anasikiliza muziki baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Celta Vigo jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  MECHI ZILIZOSALIA ZA MANCHESTER UNITED 

  Mei 7 vs Arsenal (ugenini)
  Mei 11 vs Celta Vigo (nyumbani)
  Mei 14 vs Tottenham (ugenini)
  Mei 17 vs Southampton (ugenini)
  Mei 21 vs Crystal Palace (nyumbani)
  Mei 24 - Europa League Fainali 
  KOCHA wa Manchester United, Mreno Jose Mourinho amesema kwamba atawapumzisha baadhi ya wachezaji wake katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Arsenal Jumapili.
  Kikosi cha Manchester United kimerejea Alfajiri ya leo nyumbani baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Celta Vigo 1-0 usiku wa jana kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya UEFA Europa League, bao pekee la Marcus Rashford kwa shuti la mpira wa adhabu.
  Kinda huyo wa umri wa miaka 19 aliwasili akiwa amepachika 'earphones' masikioni mwake na ingawa bao lake pekee la ugenini linaipa United nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano, lakini bado Mourinho anataka kupumzisha baadhi ya wachezaji Jumapili dhidi ya Arsenal.
  Safari ya Arsenal ni muhimu katika vita ya kuwania kuwamo ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, lakini Mreno huyo anafahamu shughuli haijakamilika katika michuano hiyo, inayotoa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwa timu inayotwaa taji.
  Alipoulizwa kama atawapumzisha baadhi ya wachezaji Uwanja wa Emirates Jumapili kuelekea mchezo wa marudiano, alisema; "Wachezaji waliopo kundini, ni wachezaji ambao wamecheza dakika nyingi, kwa sababu tumecheza mechi tisa tangu Aprili na hii, hivyo ni mechi 10 katika wiki nne na nusu.
  "Wachezaji waliopo kwenye kundi hilo, hawatacheza wikiendi ijayo," amesema.
  United inaweza kuwa imetanguliza mguu moja kwenye fainali mjini Stockholm, lakini bado watalazimika kupambana katika mchezo wa marudiani dhidi ya timu ya La Liga yenye ukuta imara.
  "Sergio (Alvarez, kipa wa Celta) aliokoa mapigo kadhaa ya hatari na kwa jinsi tulivyouanza mchezo na tulivyoutawala kipindi cha kwanza, nafikiri tulistahili matokeo mazuri," alisema Mourinho na kuongeza; "Lakini wapinzani walikuwa wagumu, mechi ilikuwa ngumu, Uwanja ulikuwa mgumu, hivyo siwezi kufurahia kazi ya wachezaji,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOURINHO KUWAPUMZISHA NYOTA WAKE MECHI NA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top