• HABARI MPYA

  Wednesday, October 19, 2016

  UGANDA YAPANGWA NA GHANA, MISRI FAINALI ZA AFRIKA 2017 GABON

  UGANDA imepangwa Kundi D pamoja na Ghana, Mali na Misri katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mapema mwakani nchini Gabon.
  Katika droo iliyopangwa usiku wa leo mjini Libreville Gabon, Uganda imejikuta inawekwa pamoja na wapinzani wake wawili wa Kundi E katika kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi, Ghana na Misri. 
  Timu nyingine katika Kundi E kuwania tiketi ya Urusi 2018, Kongo haijafuzu AFCON ya mwakani Gabon.
  Wenyeji, Gabon wamepangwa na Burkina Fasso, Cameroon na Guinea Bissau, wakati mabingwa watetezi, Ivory Coast wamepangwa pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Morocco na Togo.
  Kundi C linaundwa na Algeria, Tunisia, Senegal na Zimbabwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA YAPANGWA NA GHANA, MISRI FAINALI ZA AFRIKA 2017 GABON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top