• HABARI MPYA

  Wednesday, October 19, 2016

  AZAM FC YACHEZA MECHI YA SITA BILA USHINDI LIGI KUU, SARE 1-1 NA MTIBWA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imecheza mechi ya sita mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara bila ushindi, kufuatia kulazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mara ya mwisho, Azam ilishinda mechi ya Ligi Kuu Septemba 10, mwaka huu ilipoilaza 2-1 Mbeya Uwanja wa Sokoine.
  Kutoka hapo, ikafungwa 1-0 na Simba Septemba 17, 2-1 na Ndanda FC mjini Mtwara Septemba 24, sare ya 2-2 na Ruvu Shooting Chamazi Oktoba 2, kabla ya kufungwa 1-0 na Stand United mjini Shinyanga Oktoba 12 na sare ya 0-0 na Yanga Oktoba 16 Dar es Salaam. 
  Mara ya mwisho, Azam ilishinda mechi ya Ligi Kuu Septemba 10, mwaka huu ilipoilaza 2-1 Mbeya Uwanja wa Sokoine

  Katika mchezo wa leo, Mtibwa Sugar walianza kupata bao lililofungwa na mshambuliaji wake, Rashid Mandawa dakika ya pili, kabla ya kiungo Himid Mao kuisawazishia Azam kwa penalti dakika ya 11.
  Penalti hiyo ilitolewa baada ya mchezaji mmoja wa Mtibwa Sugar kuunawa mpira kwenye boksi na kwa matokeo hayo, Azam FC inajiongezea pointi moja na kufikisha 13 baada ya kucheza mechi 10.
  Mtibwa Sugar inafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi 11. Mechi nyingine za leo, Yanga SC imeshinda 2-0 dhidi ya Toto Africans mjini Mwanza, Ruvu Shooting imetoa sare ya 1-1 na Mwadui, Ndanda
  1-1 na Mbeya City mjini Mtwara, Prisons imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Stand United na African Lyon imefungwa 2-0 na Maji Maji, wakati kesho Simba watakuwa wenyeji wa Mbao FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHEZA MECHI YA SITA BILA USHINDI LIGI KUU, SARE 1-1 NA MTIBWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top