• HABARI MPYA

    Monday, October 24, 2016

    PLUIJM AKATAA UKURUGENZI YANGA, AAMUA KUONDOKA KIMOJA AKISEMA…

    Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amejiuzulu pamoja na benchi lake zima na amesema hataki kufanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi.
    Amesema hatua hiyo inatokana na uongozi wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina bila kumtaarifu, akisema huko ni kumvunjia heshima.
    Akizugumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo, Pluijm amesema kwamba alipaswa kutaarifiwa na uongozi juu ya jambo lolote kuhusu nafasi yake kazini, lakini ajabu anajua kupitia vyombo vya habari. 
    Pluijm amejiuzulu pamoja na benchi lake zima na amesema hataki kufanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi

    “Nimejiuzulu na sitafanya kazi tena Yanga. Ninafuatilia haki zangu na baada ya hapo nitaondoka,”alisema. Zaidi Pluijm amekerwa na kitendo cha uongozi kuleta kocha mpya yeye akiwa kazini. “Sijaambiwa chochote. Uongozi umenivunjia heshima sana, kwa klabu kama Yanga SC hawakupaswa kufanya hivyo,”alisema Pluijm.
    Aidha, kuhusu uwezekano wa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Pluijm alisema; “Sipendelei hiyo kazi. Nataka kufanya kazi na wachezaji kila siku kwa matakwa ya moyo wangu. Ninaondoka, mimi ni kocha mkubwa na nina wasifu mzuri. Nitapata timu,”alisema.
    Pluijm anaondoka siku mbili kabla ya Yanga kucheza na JKT Ruvu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumatano.
    Yanga imerejea leo kutoka Mwanza, ilikopita ikitokea Bukoba, mkoani Kagera ambako Jumamosi ilishinda 6-2 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.⁠
    Uongozi wa Yanga unamuondoa Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kumpa nafasi Mzambia, George Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.  
    Ikumbukwe, Pluijm yupo katika kipindi cha pili kufundisha Yanga baada ya awali kufundisha kwa nusu msimu mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts.
    Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari mwaka jana. 
    Saudi Arabia ambako alikwenda na aliyekuwa Msaidizi wake, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa – Pluijm  aliondoka baada ya kutofautiana na uongozi wa timu uliotaka kumsajilia wachezaji asiowataka.
    Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm alizaliwa Januari 3 mwaka 1949 na alianzia kwenye kucheza soka akiwa kipa.
    Enzi zake aliidakia kwa miaka 28 klabu ya FC Den Bosch akicheza mechi 338 ndani ya misimu 18 na alipostaafu baada ya kuumia goti akawa kocha wa timu hiyo.
    Alianza vyema ukocha akiiwezesha FC Den Bosch kutwaa ubingwa wa Daraja la Kwanza na kupanda Ligi Kuu na ndiye aliyempa nafasi ya kwanza mshambuliaji Ruud van Nistelrooy akiwa kinda wa miaka 17 tu kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
    Aprili mwaka 1995, alisaini Mkataba wa miaka miwili na SBV Excelsior kabla ya kutimuliwa Januari 1997 na nafasi yake ikachukuliwa na Msaidizi wake, John Metgod. 
    Hiyo ilifuatia timu hiyo ya Rotterdam kushinda mechi mbili tu na sare tatu katika mechi 17 za msimu mzima.
    Baada ya kuboronga Ulaya, ndipo akahamia Afrika mwaka 1999, alipokwenda kufundisha Ashanti Gold SC ya Ghana, akianza na Mkataba wa mwaka mmoja. 
    Ajax ya Uholanzi ikanunua hisa katika klabu hiyo Ijumaa ya Juni 18, mwaka 1999 asilimia 51 naye akatupiwa virago na kuhamia Saint-George SA ya Ethiopia kabla ya mwaka 2010 kujiunga na B-Juniors Feyenoord ya Ghana, ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.
    Mwaka 2012 alijiunga na Berekum Chelsea ambako pia alifukuzwa mwaka juzi na kuhamia Medeama ya Ghana pia ambako nako alifukuzwa baada ya mechi saba tu, kufuatia matokeo mabaya mwanzo mwa msimu, akivuna pointi nane kati ya 21.
    Pluijm anaondoka Jangwani baada ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 124, akishinda 77, sare 25 na kufungwa 22.
    Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 106 za tangu mwaka jana, alisema 66, sare 19 na kufungwa 20. Na anaondoka baada ya msimu mzuri uliopita, akibeba mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).
    Pluijm pia aliiwezesha Yanga kufika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 na mara ya pili kihistoria. Yanga ilifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu baada ya mwaka 1998 kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
    Na kwa mafanikio hayo, haikuwa ajabu Pluijm akishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu uliopita. 

    Kutoka kulia Juma Pondamali, Hafidh Saleh, Juma Mwambusi na Pluijm 

    REKODI YA PLUIJM YANGA SC
               P W L D
    2014 19 11 2 6
    Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki)
    Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki)
    Yanga SC 2-1 Ashanti United (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
    Yanga SC 5-2 Komorozine (Ligi ya Mabingwa )
    Yanga SC 7-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu ya Bara)
    Yanga SC 1-0 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa)
    Yanga SC 0-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa. Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)
    Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar  (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)
                          P W L D
    Tangu 2015 105 66 20 19
    Yanga SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Bara)
    Yanga SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 4-0 Polisi (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar )
    Yanga SC 1-0 Shaba (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 0-1 JKU (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 0-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
    Yanga SC 0-0 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 BDF XI (Yanga SC 1-2 BDF (Kombe la Shirikisho nyumbani)
    Yanga SC 3-0 Priosns (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-2 BDF (Kombe la Shirikisho ugenini)
    Yanga SC 0-1 Simba SC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-1 Platinum FC (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Yanga SC 0-1 FC Platinum (Kombe la Shirikisho Zvashavane)
    Yanga SC 8-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
    Yanga SC 1-1 Etoile du Sahel (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 3-2 Stand United (Ligi Kuu)
    Yanga SC 5-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
    Yanga SC 4-1 Polisi Moro
    Yanga SC 0-1 Etoile du Sahel (Kombe la Shirikisho)
    Yanga SC 1-2 Azam FC (LIgi Kuu)
    Yanga SC 0-1 Ndanda FC (Ligi Kuu)
    Yanga SC 3-2 Friends Rangers (Kirafiki Karume)
    Yanga SC 0-0 SC  Villa (Kirafiki Taifa)
    Yanga SC 1-0 KMKM (KIrafiki Taifa)
    Yanga SC 3-0 Polisi Kombaini (KIrafiki Taifa)
    Yanga SC 1-2 Gor Mahia (Kagame Taifa)
    Yanga SC 3-0 Telecom (Kagame Taifa)
    Yanga SC 1-0 Khartoum N (Kagame Taifa)
    Yanga SC 0-0 Azam FC pen (3-5 Robo Fainali Kagame Dar)
    Yanga SC 4-1 Kemondo FC (Kirafiki Mbozi. Mbeya)
    Yanga SC 2-0 Prisons (Kirafiki Mbeya)
    Yanga SC 3-2 Mbeya City (Kirafiki Mbeya)
    Yanga SC 0-0 Azam FC (8-7 penalti Ngao ya Jamii)
    Yanga SC 2-0 Coastal Union (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 3-0 Prisons (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 4-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu Taifa) 
    Yanga SC 2-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 4-1 Toto Africans (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-2 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)
    Yanga SC 2-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Tabora)
    Yanga SC 0-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu Mkwakwani)
    Yanga SC 1-0 African Sports (Ligi Kuu Mkwakwani)
    Yanga SC 4-0 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 4-2 Friends Rangers (Kirafiki Boko)
    Yanga SC 3-0 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 3-0 Mafunzo (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 2-1 Mtibwa Sugar (Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 1-1 URA (URA ilishinda kwa penalti 4-3 Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Yanga SC 1-0 Ndanda (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 5-0 Majimaji FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 3-0 Majimaji FC (Kombe la TFF Taifa)
    Yanga SC 0-2 Coastal Union (Ligi Kuu Mkwakwani)
    Yanga SC 2-2 Prisons (Ligi Kuu Sokoine, Mbeya)
    Yanga SC 4-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 1-0 Cercle de Joachim (Ligi ya Mabingwa Mauritius)
    Yanga SC 2-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Kombe la TFF Taifa)
    Yanga SC 2-0 Cercle de Joachim (Ligi ya Mabingwa Taifa)
    Yanga SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 5-0 African Sports (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 APR (Ligi ya Mabingwa Amahoro, Kigali)
    Yanga SC 1-1 APR (Ligi ya Mabingwa Taifa, Dar)
    Yanga SC 2-1 Ndanda FC (Kombe la TFF Taifa)
    Yanga SC 3-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa, Taifa)
    Yanga SC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-2 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa, Alexandria)
    Yanga 2-1 Coastal Union (Kombe la TFF, Mkwakwani, mechi ilivunjika dakika ya 110 Yanga ikiwa inaongoza 2-1 baada ya mashabiki wa Coastal kumjeruhi kwa jiwe mshika kibendera namba mbili, Charles Simon wa Dodoma. Siku tatu baadaye, TFF ikaiidhinisha Yanga kucheza fainali)
    Yanga SC 2-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 2-1 Toto Africans (Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga SC 3-1 Toto Africans (Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga SC 2-0 Sagrada Esperanca (Kombe la Shirikisho Afrika Taifa)
    Yanga SC 2-0 Mbeya City (Ligi Kuu Sokoine)
    Yanga SC 2-2 Ndanda FC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 0-1 Sagrada Esperanca (Kombe la Shirikisho Afrika Angola)
    Yanga 2-2 Majimaji (Ligi Kuu Songea)
    Yanga 3-1 Azam FC (Fainali Kombe la TFF Taifa)
    Yanga 0-1 MO Bejaia (Kundi A Kombe la Shirikisho Bejaia)
    Yanga 0-1 TP Mazembe (Kundi A Kombe la Shirikisho Taifa)
    Yanga 1-1 Medeama (Kundi A Kombe la Shirikisho Taifa)
    Yanga 1-3 Medeama (Kundi A Kombe la Shirikisho Ghana)
    Yanga 0-0 Mtibwa Sugar (Kirafiki Taifa)
    Yanga 1-0 MO Bejaia (Kundi A Kombe la Shirikisho)
    Yanga 2-2 Azam FC (Penalti 1-4 Ngao ya Jamii Taifa)
    Yanga 1-3 TP Mazembe (Kundi A Kombe la Shirikisho Lubumbashi)
    Yanga 3-0 African Lyon (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 0-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara)
    Yanga 3-0 Maji Maji FC (Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga SC 2-0 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)
    Yanga SC 0-1 Stand United (Ligi Kuu Shinyanga)
    Yanga 1-1 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 3-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 0-0 Azam (Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 2-0 Toto Africans (Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga 6-2 Kagera Sugar (Ligi Kuu Kaitaba)
    Wachezaji wa Yanga watakuwa chini ya kocha kuanzia kesho

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM AKATAA UKURUGENZI YANGA, AAMUA KUONDOKA KIMOJA AKISEMA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top