• HABARI MPYA

    Saturday, October 22, 2016

    MANJI AFUTA MKUTANO WA KESHO, LAKINI ASEMA ATAPAMBANA NAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Manji ametii agizo la Mahakama kwa kuufuta Mkutano Mkuu wa dharula wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika kesho makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana ilitoa katazo la kufanyika Mkutano wa kesho kufutia kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.
    Manji ametangaza kuufuta Mkutano huo mchana wa leo akizungumza na Waandishi wa Habari Jangwani.
    Na amesema taratibu za kisheria zinafanyika juu ya kupambana na pingamizi hilo ili liondolewe na tarehe nyingine ya Mkutano itatajawa mara mpango huo utakapofanikiwa.
    Kwa mujibu wa hati ya agizo halali la Mahakama, uongozi wa Yanga umezuiwa kufanya Mkutano huo baada ya kesi iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji na Kampuni ya Yanga Yetu.
    Ajenda kuu ya Mkutano huo ilikuwa ni kupitisha Baraza la Wadhamini la klabu hiyo pamoja na kuondoa Mjumbe mmoja na kuweka mpya.
    Na hayo yanafuatia Baraza la Wadhamini kuikodisha timu kwa kampuni ya Yanga Yetu kwa miaka 10, baada ya wanachama kuafiki ombi la Mwenyekiti wao, Yussuf Manji katika Mkutano wa Agosti 6, mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI AFUTA MKUTANO WA KESHO, LAKINI ASEMA ATAPAMBANA NAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top