• HABARI MPYA

    Thursday, October 27, 2016

    MAREFA WA KIKE WAMEGEWA SHAVU LIGI YA WANAWAKE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAREFA wa kike ndiyo watakaopewa nafasi zaidi kuchezesha Ligi ya soka la Wanawake Tanzania, inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba Mosi katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma huku viwanja vitatu vikitarajiwa kuwaka moto. 
    Hayo yamesemea na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alipokuwa anazungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Saaalam jana Dar es Salaam.
    Ligi huyo inayotarajiwa kuanza Novemba 1, mwaka huu kuwa wanaamini katika uzinduzi huo utakuwa wa pekee kwa sababu utahudhuriwa na wabunge wa Bunge la Tanzania.
    Jonesia Rukyaa wa pili kushoto ni miongoni mwa marefa wa kike wenye uzoefu mkubwa

    Ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na kuwakikishwa na nyota mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara imegawanyika katika makundi A na Bekee kwa sababu utahudhuriwa na wabunge wa Bunge la Tanzania.
    Alizitaja timu ambazo zitafungua ligi hiyo kuwa ni Baobao Queens ya Dodoma itawakaribisha Victoria ya Iringa mchezo ambao utacgezwa uwanja wa Jamhuri Dodoma, Marsh ya Mwanza itakuwa wageni wa Majengo ya Kigoma Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
    Mchezo mwingine utakuwa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ambapo wenyeji JKT Queens watakuwa wenyeji wa Mlandizi Queens.
    Alisema kuwa benchi la ufundi la timu ya taifa ya wanawake, litagawanywa katika mikoa hiyo ili kuangalia wachezaji wenye uwezo ambao wataunda kwenye kikosi cha timu ya taifa.
    "Timu ya taifa itatolewa na mashindano haya, hatutakuwa na wachezaji wale wale kila siku na pia ligi hii itatisaidia kupata kikosi cha vijana U-20," alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA WA KIKE WAMEGEWA SHAVU LIGI YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top