• HABARI MPYA

    Sunday, October 30, 2016

    HUO UBISHI WA MBAO HATA KWA YANGA, AU ILIKUWA KWA SIMBA TU?

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC wanateremka kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam jioni ya leo kumenyana na Mbao FC ya Mwanza katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mchezo huo unakuja siku mbili baada ya uongozi kughairi mpango wa kumuachia kocha wake, Mholanzi Hans van der Pluijm aondoke. 
    Yanga juzi ilimuandikia barua ya kumuomba kurudi kazini kocha wake, Mholanzi Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm. 
    Mholanzi huyo alijiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina bila kumtaarifu, akisema huko ni kumvunjia heshima.
    Mbao iliwatoa jasho Simba SC walioshinda 1-0 kwa mbinde bao la dakika za jioni la kiungo Muzamil Yassin 

    Kocha huyo akakataa hadi nafasi ya Ukurugenzi wa Ufundi amabyo inasemekana Yanga ilitaka kumpa baada ya kumleta Lwandamina kuwa kocha Mkuu.
    Lakini baada ya kuwaaga wachezaji siku moja kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKR Ruvu timu ikishinda 4-0 Jumatano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliingilia kati suala hilo.
    Waziri Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, kwanza aliushauri uongozi kumrudisha Pluijm na baadaye akaenda kuzungumza na kocha huyo pia kumshauri akubali kurejea.
    Baadaye akazikutanisha pande zote mbili, Pluijm na uongozi wa Yanga katika kikao ambacho inaelezwa makubaliano yalifikiwa na wawili kuamua kurejeana.
    Uongozi wa Yanga ulitaka kumuondoa Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.  
    Pluijm sasa anaendeleza rekodi yake nzuri aliyoiacha ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 124, akishinda 77, sare 25 na kufungwa 22.
    Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 106 za tangu mwaka jana, alisema 66, sare 19 na kufungwa 20.
    Hata hivyo, Mholanzi huyo leo ana mtihani mgumu kidogo, kwani Mbao inaonekana na timu ngumu ambayo iliwatoa jasho hadi vinara wa Ligi Kuu msimu huu, Simba SC walioshinda 1-0 kwa mbinde bao la dakika za jioni la kiungo Muzamil Yassin. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HUO UBISHI WA MBAO HATA KWA YANGA, AU ILIKUWA KWA SIMBA TU? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top