• HABARI MPYA

  Wednesday, October 19, 2016

  NA LEO TAMBWE HAYUMO KABISAA KIKOSINI YANGA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  YANGA itaendelea kumkosa tegemeo lake la mabao, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Kikosi cha timu ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kwa ajili ya mchezo wa jioni ya leo kimekwishatoka na kwa mara ya pili mfululizo washambuliaji wa zamani wa FC Platinums ya Zimbabwe, Donald Ngoma na Obrey Chirwa wameanzishwa pamoja.
  Mzimbabwe Ngoma aliye katika msimu wake wa pili Yanga alianzishwa na Mzambia Chirwa aliyesajiliwa msimu huu katika mchezo uliopita timu hiyo ikilazimishwa sare ya 0-0 na Azam FC. 
  Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Deo Munishi 'Dida', Hassan Kessy, Oscar Joshua, Andrew Vincent 'Dante', Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Ngoma, Chirwa na Deus Kaseke.
  Katika benchi wapo; Beno Kakolanya, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub 'Cannavaro', Saidi Juma 'Makapu', Thabani Kamusoko, Matheo Anthony na Juma Mahadhi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NA LEO TAMBWE HAYUMO KABISAA KIKOSINI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top