• HABARI MPYA

  Wednesday, October 19, 2016

  CHIPPA YA SAUZI YAMTAKA KICHUYA, YATUMA MTU KUJA KUMALIZANA NAYE DAR

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  WAKALA wa wachezaji, Rodgers Mathaba atatua nchini baadaye mwezi huu kwa mpango wa kumpeleka klabu ya Chippa United FC ya Afrika Kusini, winga wa Simba SC, Shizza Ramadhani Kichuya.
  Mathaba anakuja kuzungumza na Simba SC pamoja na mchezaji huyo juu ya ofay a Chippa kwenda kucheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
  Mathaba aliiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana kwa simu kutoka Afrika Kusini kwamba Chippa imevutiwa na Kichuya na iko tayari kumnunua. “Ninakuja Dar es Salaam kujaribu kukamilisha huo mpango, kuona kama Simba watakuwa tayari kumuuza Kichuya, kijana mwenye kipaji sana,”alisema.   
  Winga wa Simba SC, Shizza Ramadhani Kichuya anatakiwa na Chippa United ya Afrika Kusini

  Mathaba ambaye Julai mwaka huu alifanikiwa kumuunganisha mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib na klabu ya Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini pia, alisema akiwa nchini atazungumza na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  “Nitazungumza na TFF kwa sababu nimataka kujadiliana nao namna ya kuwasaidia wachezaji chipukizi wa Tanzania kwenda kukomzwa nje,”alisema.
  Kichuya yupo katika msimu wake wa kwanza Simba SC baada ya kusajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro – lakini tayari ametokea kuwa tegemeo la mabao la Wekundu hao wa Msimbazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIPPA YA SAUZI YAMTAKA KICHUYA, YATUMA MTU KUJA KUMALIZANA NAYE DAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top