• HABARI MPYA

    Thursday, June 02, 2016

    STARS WALIVYOJIFUA LEO MAZOEZI YA 'MWISHO MWISHO' KABLA YA KUWAVAA MAFARAO

    Winga wa Azam FC, akipasua katikati ya kiungo wa Coastal Union, Juma Mahadhi (kulia) na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vincent 'Dante' wakati wa mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri, Jumamosi
    Nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta (kushoto) akigombea mpira na kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohammed 'Mo' Ibrahim leo kwenye mazoezi ya timu ya taifa

    Kiungo wa akimiliki mpira mbele ya Deus Kaseke wa Yanga na Mwinyi Kazimoto wa Simba (nyuma) leo Uwanja wa Taifa

    Beki wa Azam FC, David Mwantika (juu) akipambana na mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguli leo

    Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib akimtoka kiungo wa Azam FC, Himid Mao

    Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto (mbele) akipambana na kiungo mwenzake wa Simba SC, Jonas Mkude leo

    Samatta (kulia) akiwania mpira dhidi ya Mwantika leo Uwanja wa Taifa

    Jonas Mkude akiambaa na mpira mbele ya Farid Mussa

    Kipa wa Yanga, Deo Munishi 'Dida' akimnyoosha viungo mlinda mlango wa Azam FC, Aishi Manula. Kulia ni kocha wa makipa wa Stars, Manyika Peter

    Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa akimpa maelekezo beki anayeweza kucheza kama kiungo wa Azam FC, Erasto Nyoni leo 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS WALIVYOJIFUA LEO MAZOEZI YA 'MWISHO MWISHO' KABLA YA KUWAVAA MAFARAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top