• HABARI MPYA

    Friday, June 24, 2016

    TYSON FURY AUMIA MAZOEZINI, AJITOA PAMBANO LA MARUDIANO NA KLITSCHKO

    BONDIA Tyson Fury amejitoa kwenye pambano la kutetea mikanda yake ya dunia ya WBO, WBA na IBO uzito wa juu na Wladimir Klitschko mwezi ujao baada ya kuumia kifundo cha mguu.
    Bingwa huyo wa dunia aliyeumia wakati anafanya mazoezi ya kukimbia eneo la Lake District, ametangaza kuahirisha pambano hilo lililokuwa lifanyike Julai 9 mjini Manchester, England.
    Fury amesema: "Kiasi cha siku 10 zilizopita nilikuwa ninakimbia Lake District na nikaangukia kifundo cha mguu na kuumia.  Nimekwenda hospitali na kufanyiwa vipimo vya MRI na X-Rayf. Sijavunjika, lakini ni maumivu makubwa na nimeambiwa kupumzika kwa wiki sita saba,".


    Tyson Fury amejitoa kwenye pambano la marudiano na Wladmir Klitschko baada ya kuumia enka
     
    PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    "Nilijaribu kuendelea na mazoezi hivyo hivyo, ili kupata maoni mengine wiki moja baadaye, lakini ni ushauri ule ule, hivyo pambano litaahirishwa," amesema.
    Fury - anayejulikana kwa jina la utani 'The Gypsy King' - alimaliza utawala wa zaidi ya muongo mzima wa Klitschko kama bingwa wa uzito wa juu wa ndondi za kulipwa duniani baada ya kumshinda kwa pointi ukumbi wa Esprit Arena mjini Dusseldorf, Ujerumani Novemba mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TYSON FURY AUMIA MAZOEZINI, AJITOA PAMBANO LA MARUDIANO NA KLITSCHKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top