• HABARI MPYA

    Sunday, June 26, 2016

    MAZEMBE WATUA, ULIMWENGU ASEMA; “TUMEKUJA KUWAFUNGA TATU YANGA”

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidekorasia ya Kongo (DRC) kimewasili usiku huu na mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amepata mapokezi mazuri.
    Watu kadhaa walimlaki Ulimwengu baada ya kutokeza nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Mazembe ilipowasili kwa ajili ya mchezo wa keshokutwa dhidi ya wenyeji, Yanga. 
    Aidha, Ulimwengu alionyesha ishara ya vidole vitatu wakati mashabiki wanamlaki, akimaanisha watawafunga Yanga mabao tatu.
    Thomas Ulimwengu (katikati) akionyesha ishara ya vidole vitatu baada ya kuwasili na JNIA na kikosi cha Mazembe
    Mabingwa hao mara tano wa Afrika watamenyana na Yanga katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Na mara baada ya kuwasili, Ulimwengu alisema; “Tunamshukuru Mungu tumefika salama, tumekuja kucheza na timu bora, Yanga tunaiheshimu, lakini tutapmbana tushinde ili tujiweke katika mazingira mazuri ya kwenda fainali,”alisema.
    Ulimwengu alisema anaifahamu Yanga na wachezaji wake wengi ambao yupo nao timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni timu nzuri na mchezo utakuwa mgumu Jumanne.
    Mazembe imekuja na kikosi cha wachezaji 18 ambao ni; Robert Kidiaba, Sylvain Gbohou, Issama Mpeko, Joel Kimwaki, Thomas Ulimwengu, Christian Koume,
    Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope,
    Jose Badibake, Kissi Boateng, Roger Assale, Rainford Kalaba, Deo Kanda, Adama Traore, Chriastian Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.
    Maofisa wa benchi la Ufundi wanaokuja ni Theobald Binamungu, Mohamed Kamwanya,
    Dony Kabongo, Frederic Kitengie na Andre Ntime.
    Madaktari ni Hurbert Velud, Pamphile Mihayo, Mhudumu Richard Mubemb na Maofisa wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Heritier Yinduka, Arther Kikuni na Meshack Kayembe.
    Ulimwengu katikati akitembea kibabe baada ya kuwasili Dar ea Salaam 
    Mashabiki wapiga picha na Ulimwengu baada ya kuwasili na Mazembe Dar es Salaam
    Wachezaji wengine wa Mazembe wakitoka nje ya JNIA baada ya kutua Dar es Salaam 

    Makocha wa Mazembe walikuwa wa kwanza kutoka nje ya JNIA baada ya timu kuwasili

    Katika mechi za kwanza za kundi hilo, Mazembe ilishinda 3-1 nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana wakati Yanga ilifungwa 1-0 ugenini na MO Bwejaia ya Algeria Jumapili iliyopita.
    Waamuzi wa mchezo huo ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZEMBE WATUA, ULIMWENGU ASEMA; “TUMEKUJA KUWAFUNGA TATU YANGA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top