• HABARI MPYA

    Wednesday, June 22, 2016

    MMILIKI WA TP MAZEMBE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA

    MMILIKI wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Moise Katumbi amehukimiwa kifungo cha miaka mitatu jela.
    Mfanyabiashara huyo tajiri, amekumbwa na adhabu hiyo yeye mwenyewe akiwa nje ya nchi kwa matibabu.
    Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 51 amekutwa na hatia ya kujimilikisha na kuuza jengo kinyume cha sheria mjini Lubumbashi, ambako ni ngome yake kuu ya kisiasa.
    Na hayo yanatokea wakati tayari amependekezwa na vyama vya sita vya siasa kugombea Urais wa DRC unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.
    Mmiliki wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Moise Katumbi amehukimiwa kifungo cha miezi 36 jela

    Rais Joseph Kabila, ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2001, anakaribia kumaliza kipindi chake cha pili cha utawala na kwa mujibu wa Katiba anatakiwa kustaafu Desemba.
    Lakini kuna hisia kwamba hukumu hiyo ni shinikizo za kisiasa ili kumvunja nguvu Katumbi, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa Rais mpya wa DRC.
    Mahakama ya Lubumbashi, mji wa pili kwa ukubwa DRC, pia imempiga faini ya dola za KImarekani Milioni 4.1 kwa kosa la kuuza jengo hilo ambalo raia huyo wa Ugiriki amesema ni mali ya famili yake.
    Katumbi alisafiri nje ya nchi Mei 20, mwaka huu wakati tayari imekwishatolewa hatu ya kukamatwa kwake.
    Katumbi anatarajiwa kukatia rufaa hukumu hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MMILIKI WA TP MAZEMBE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top