• HABARI MPYA

    Friday, June 24, 2016

    ES SETIF YAONDOLEWA LIGI YA MABINGWA KWA VURUGU ZA MASHABIKI

    TIMU ya ES Setif ya Algeria imeondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, kufuatia vurugu kubwa zilizofanywa na mashabiki wake katika mchezo na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wiki iliyopita.
    Taarifa ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) kwa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE imesema kwamba kufuatia tukio hilo katika mchezo namba 98 wa 2016, amnao marefa walilazimika kuusitisha kabla ya kumalizika, Setif imeadhibiwa.

    Ripoti ya marefa imesema amani ilichafuka uwanjani baada ya mashabiki kurusha mioto, chupa na mawe na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa kabla ya walinzi kuingilia kati kutuliza hali hiyo.
    Kwa sababu hiyo, kwa kutimia ibara ya saba ibara ya tatu ya kanuni za mashindano, Kamati ya Maandalizi ya michuano ya klabu ya CAF imeifuta ES Setif  na hatua zaidi zitachukuliwa na Bodi ya Nidhamu ya shirikisho hilo.
    Ibara ya saba kanuni ya tatu inasema: “3. Iwapo refa atalazimika kuvunja mchezo kabla ya kumalizika muda wa kawaida kwa sababu ya vurugu uwanjani, timu mwenyeji itapoteza mchezo na inaweza kuondolewa kwenye mashindano,”.
    Na baada ya maamuzi hayo, Kundi B sasa linabaki na timu tatu na Zamalek ndiyo inaongoza kwa pointi zake tatu wakati Enyimba na Mamelodi hazina pointi. 
    MSIMAMO WA KUNDI B BAADA YA KUONDOLEWA ES SETIF
    Timu
    P/J
    W/G
    D/N
    L/P
    GF
    GA
    GD
    Total

    Zamalek
    1
    1
    -
    -
    1
    0
    +1
    3

    Enyimba
    1
    -
    -
    1
    0
    -1
    -1
    0

    Mamelodi

    Sundowns
    -
    -
    -
    -
    -
    -
    -
    0
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ES SETIF YAONDOLEWA LIGI YA MABINGWA KWA VURUGU ZA MASHABIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top