• HABARI MPYA

    Wednesday, June 29, 2016

    KOCHA ATAJA KIKOSI CHA TWIGA STARS KITAKACHOHEZA NA RWANDA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanawake, maarufu Twiga Stars, Nasra Juma ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaokwenda Kigali, Rwanda Julai 15 kucheza na Rwanda mechi ya kirafiki.
    Twiga Stars inakwenda Rwanda kwa mchezo huo kufutia mwaliko wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), kupamba Mkutano wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) na Rais wa Rwanda, mpenzi maarufu wa soka anagtarajiwa kuwa mgeni rasmi.
    Fatma Issa (kulia) ameitwa Twiga Stars itakayoivaa Rwanda
    Kikosi cha Twiga kilichoitwa kwa ajili ya mchezo huo ni makipa; Fatma Omary, Belina Julius na Najiat Abbas.
    Mabeki Stumai Abdallah, Fatma Issa, Anastazia Antony, Happyness Henziron na Maimuna Khamis.
    Viungo ni Donisia Daniel, Amina Ali, Amina Ramadhani, Fatuma Bashiri, Wema Richard, Fadhila Hamadi
    Mwajuma Abdallah, Anna Hebron na Sophia Mwasikili.
    Washambuaji ni Tumaini Michael, Johari Shaaban, Fatma Idd, Shelder Boniface Mafuru, Asha Saada Rashid na Mwanakhamisi Omar 'Gaucho'.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA ATAJA KIKOSI CHA TWIGA STARS KITAKACHOHEZA NA RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top