• HABARI MPYA

    Tuesday, June 28, 2016

    MAGETI YAFUNGWA, WATU WA NJE WATIMULIWA KWA MABOMU UWANJA WA TAIFA

    Askari Polisi (kushoto) akiwafukuza mashabiki waliojitokeza kuingia bure kwenye mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga na TP Mazembe ya DRC kuondoka baada ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kusheheni watu zaidi ya idadi iliyotakiwa, watazamani 40,000
    Askari Polisi akiwa amesimama imara dhidi ya raia ambao bado hawajakata tamaa kuingia uwanjani
    Askari zaidi wa Jeshi la Polisi wakipewa mwongozo namna ya kuwadhibiti mashabiki
    Raia wakiwa nje ya geti kabla ya kuodolewa kwa mabomu ya machozi
    Askari huyu alilazimika kumtandika ngumi shabiki aliyetaka kulazimisha kuingia licha ya kuzuiwa
    Uwanja wa Taifa kama unavyoonekana hadi kufika Saa 7:00 mchana 
    Mashabiki wa wa wapinzani, Simba wamejitokeza katika nafasi zao ili kuwashangilia wageni, TP Mazembe
    Haijulikani sababu ya eneo hili kuachwea wazi. Watu wamezuiwa kukaa hapa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAGETI YAFUNGWA, WATU WA NJE WATIMULIWA KWA MABOMU UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top