• HABARI MPYA

    Tuesday, June 28, 2016

    OSCAR NJE, MBUYU TWITE KUCHEZA BEKI YA KUSHOTO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA itacheza mechi yake ya pili ya Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC bila beki halisi wa kushoto, kufuatia Oscar Joshua kushindwa kupata nafuu.
    Oscar aliumia kipindi cha kwanza na kumpisha Miwnyi Hajji Mngwali katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo Juni 19 mjini nchini Algeria Yanga ikifungwa 1-0 na wenyeji MO Bejaia.
    Mngwali akapewa kadi mbili mfululizo za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90, hivyo kuondolewa kwenye mchezo wa leo.
    Mbuyu Twite atacheza beki ya kushoto leo dhidi ya TP Mazembe ya kwao, DRC

    Benchi la Ufundi la Yanga chini ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm lilijaribu kumlazimisha Oscar acheze mechi ya leo kwa kumfanyisha mazoezi baada ya siku mbili.  
    Hata hivyo, kufikia jana Pluijm akajiridhisha kwamba Oscar hawezi kucheza leo na ameamua atampanga kiungo Mbuyu Twite katika upande huo.
    Kwa kawaida Twite amekuwa akicheza nafasi za beki wa kulia, beki wa kati na kiungo wa ulinzi tangu anacheza kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na baadaye Rwanda – lakini leo kwa mara ya kwanza atacheza beki ya kushoto. 
    Katika mechi za kwanza za kundi hilo, Mazembe ilishinda 3-1 nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana wakati Yanga ilifungwa 1-0 ugenini na MO Bejaia ya Algeria Jumapili iliyopita.
    Mchezo wa leo utachezeshwa na Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
    Ikumbukwe, wenyeji Yanga wameamua mashabiki waingie bure ili kuvutia wengi wa kushangilia timuya nyumbani dhidi ya mabingwa mara tano Afrika.
    Na Kamisa wa mchezo huo, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda amesema anataka watu 40, 000 tu badala ya 60,000 kulingana na uwezo wa Uwanja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OSCAR NJE, MBUYU TWITE KUCHEZA BEKI YA KUSHOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top