• HABARI MPYA

    Monday, June 27, 2016

    MILOVAN NDIYE KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA ALGERIA

    SASA rasmi! Shirikisho la Soka Algeria (FAF) lina kocha mpya. Ni Mserbia, Milovan Rajevac. Taarifa zimetolewa jana katika tovuti ya FAF.
    Mserbia huyo anachukua nafasi ya Christian Gourcuff, aliyejiuzulu mwenyewe kwa matakwa yake mwanzoni mwa Aprili, baada ya kusema anataka kurudi kufundisha klabu. Milovan Rajevac ataiongoza Algeria katika mechi ya kwanza rasmi Septemba dhidi ya Lesotho Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida, ambayo itakuwa ni mechi ya sita na ya mwisho ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017.
    Milovan Rajevac ndiye kocha mpya wa timu ya taifa ya Algeria

    FAF imesema kwamba kocha huyo alisaini Mkataba jana asubuhi alipokutana na Mohamed Raouraoua
    Milovan Rajevac ana uzoefu wa kufanya kazi Afrika kwa miaka miwili tu kati ya 2008 na 2010 alipofundisha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Ghana na abaadaye akapewa timu ya wakubwa aliyoiwezesha kufuzu Kombe la Dunia. 
    Alikuwepo kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika 2010 nchini Angola na Black Stars. Katika Kombe la Dunia mwaka huo huo, Rajevac aaliweka historia kwa kukaribia kuipeleka timu ya kwanza ya Afrika Nusu Fainali.
    Milovan Rajevac ataanza kazi rasmi Algeria Julai 1 na atatambulishwa rasmi Julai 12. Waliokuwa wasaidizi wa Christian Gourcuff wataendelea. Nabil Neghiz ataendelea kuwa kocha Msaidizi. Yazid Mansouri anabaki kama Meneja wa timu. Guillaume Marie ataendelea kuwa kocha wa mazoezi ya nguvu na Belhadji-Bolly ataendelea kuwa kocha wa makipa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MILOVAN NDIYE KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top