• HABARI MPYA

    Sunday, June 26, 2016

    YANGA NA MAZEMBE KIINGILIO BURE JUMANNE TAIFA

    Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imefuta viingilio katika mchezo wa Jumanne wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC na sasa mashabiki wataingia bure.
    Taarifa ya Yanga SC jioni hii imesema lengo la kufuta viingilio ni kuvutia mashabiki wengi zaidi uwanjani wajitokeze kuishangilia timu ya nyumbani dhidi ya timu kutoka DRC.
    Awali, Yanga ilitaja viingilio viwili tu katika mchezo huo ambavyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 30,000 kwa VIP na tiketi ilikuwa zianza kuuzwa kesho.
    Huo utakuwa mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
    Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa watatu kutoka nchi tatu tofauti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
    Hao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA MAZEMBE KIINGILIO BURE JUMANNE TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top