• HABARI MPYA

    Thursday, June 02, 2016

    BARCELONA YATHIBITISHA; "DANI ALVES ANAONDOKA"

    Beki wa kulia wa Brazil, Dani Alves atahitimisha miaka yake ya nane ya kucheza Barcelona msimu huu  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    MATAJI ALIYOSHINDA DANI ALVES

    La Liga: 2008–09, 2009–10, 2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015-16
    Kombe la Mfalme (Copa del Rey): 2008–09, 2011–12, 2014–15, 2015–16
    Super Cup ya Hispania: 2009, 2010, 2011, 2013
    Champions League: 2008–09, 2010–11, 2014–15
    Super Cup ya UEFA: 2009, 2011, 2015
    Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2009, 2011, 2015
    KLABU ya Barcelona imethibitisha Dani Alves ataondoka, lakini imekana kuwa na mpango wa kumchukua Hector Bellerin wa Arsenal akazibe pengo lake.
    Alves amekuwa kazini Nou Camp tangu asalijiwe kutoka Sevilla miaka nane iliyopita. 
    Mkurugenzi wa Usajili, Roberto Fernandez amesema: "Dani ameamua kuondoka na tunapaswa kukubali uamuzi wake. Ameithibitishia klabu anachotaka ni kuondoka.
    "Tunapaswa kukumbuka kwamba amemaliza Mkataba wake mwaka uliopita, lakini hatukuweza kusajili mchezaji yeyote kwa sababu ya adhabu ya kufungiwa kusajili na FIFA na hivyo yalikuwa mazingira magumu kwetu na akaongeza Mkataba. Lakini sasa anatafuta mazingira mazuri zaidi kwake,". 

    REKODI YA MSIMU HUU YA DANI ALVES 

    Mechi alizocheza: 29
    Mabao aliyofunga: 0
    Pasi za mabao alizotoa: 4
    Mipira aliyopitia miguuni mwa mabeki: 37
    *Takwimu hizi ni za La Liga pekee 
    Alves amekaribia kumalizana na Juventus na wakala wake, Dinorah Santana pia anafanya mazungumzo na Paris Saint-Germain. 
    Beki huyo wa kulia anaweza kupewa dau zuri kwa sababu katika Mkataba wake mpya, kwa sababu wakati anaongeza Mkataba Barca mwaka jana, walikubaliana vigogo hao wa Hispania hawatapa ada ya uhamisho akiondoka Camp Npu.
    Mkongwe huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 33, anaondoka Barca baada ya miaka nane, akishinda mataji 23.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCELONA YATHIBITISHA; "DANI ALVES ANAONDOKA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top