• HABARI MPYA

    Tuesday, June 14, 2016

    SERENGETI BOYS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA SHELISHELI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kinaingia kambini leo Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
    Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli na wachezaji wanaoingia kambini ni pamoja na makipa Kelvin Deogratius Kayego, Ramadhani Awm Kambwili na Samwel Edward Brazio.
    Mebeki ni Kibwana Ally Shomari, Israel Patrick Mwenda, Anton Shilole Makunga, Nickson Clement Kibabage, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi na Issa Abdi Makamba.

    Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamis Ng’anzi, Shaban Zuberi Ada, Mustapha Yusuph Mwendo, Yassin Muhidini Mohammed, Cyprian Benedictor Mtesigwa, Asad Ali Juma, Mohammed Abdallah Rashid na Muhsin Malima Makame na washambuliaji Ibrahim Abdallah Ali Henrick Vitalis Nkosi, Rashid Mohammed Chambo na Yohana Oscar Nkomola.
    Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
    Kadhalika Serengeti Boys ilicheza mfululizo michezo saba ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
    Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA SHELISHELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top