• HABARI MPYA

  Tuesday, June 14, 2016

  WAPINZANI WA YANGA WAKATA KUJITOA KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU ya Medeama SC ya Ghana inataka kujitoa katika Kundi A michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya kifedha.
  Timu hiyo inatarajiwa kuanza na waliokuwa mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya DRC Jumapili, siku ambayo Yanga ya Tanzania itakuwa mgeni wa MO Bejaia nchini Algeria katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
  Ofisa wa Mawasiliano wa Medeama, Benjamin Kessie amesema katika taarifa yake kwa Umoja wa Waandishi wa Habari Afrika, maarufu kama Football Africa Arena kwamba iwapo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) halitawasaidia fedha watajitoa. 

  Medeama kama timu zote zilizofuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani baada ya Ligi ya Mabingwa, inapaswa kupewa dola za Kimarekani 150,000.
  Hata hivyo, CAF bado haijafanya mgawo huo na timu hiyo ya Ghana ilidhani ikifuzu tu itapatiwa fedha hizo ziwasaidie kusafiri kwenda Lubumbashi, DRC kucheza na Mazembe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAPINZANI WA YANGA WAKATA KUJITOA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top