• HABARI MPYA

    Thursday, June 09, 2016

    MOURINHO AMUONGEZA MWAKA WA 11 CARRICK MAN UNITED

    KIUNGO wa England, Michael Carrick amesaini Mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea Manchester United chini ya kocha mpya, Mreno Jose Mourinho.
    Man United imsema leo kwamba kiungo huyo iliyemsajili kutoka Tottenham mwaka 2006, amekubali kuongeza Mkataba utakaomuweka Old Trafford hadi Juni 2017 kukamilisha miaka 11 ya kuwatumikia Mashetani Wekundu.
    Katika kipindin chake cha miaka 10 Man United hadi sasa, mchezaji huyo ameshinda mataji matano ya Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Ligi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA. 
    Kiungo wa England, Michael Carrick amesaini Mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuwajibika Manchester United  PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

    "Hii ni klabu kubwa na imekuwa sehemu ya maisha yangu kwa miaka 10 iliyopita, hivyo nina furaha safari hii nzuri inaendelea," amesema Carrick.
    Pia akaelezea furaha yake ya kuingia katika zama mpya za kufanya kazi na kocha mpya, Jose Mourinho ambaye aliteuliwa mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Mholanzi, Louis van Gaal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOURINHO AMUONGEZA MWAKA WA 11 CARRICK MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top