• HABARI MPYA

    Wednesday, June 15, 2016

    BRAZIL YAMTUPIA VIRAGO KOCHA DUNGA SELECAO

    BRAZIL imemfukuza kazi kocha Carlos Dunga baada ya matokeo mabaya kwenye michuano ya Copa America Centenario inayoendelea nchini Marekani.
    The Selecao wametolewa kwenye hatua ya makundi tu ya mashindano hayo baada ya kutoa sare na Ecuador na kufungwa na Peru, licha ya kushinda 7-1 dhidi ya Haiti.
    Nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na kocha wa Corinthians, Tite, ambaye ataiongoza timu hiyo katika michuano ijayo ya Olimpiki nchini Brazil.
    Dunga aliingia kwenye mashindano hayo akiwa katika wakati mgumu baada ya timu kucheza vibaya kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 na pamoja na matokeo mabaya ya Marekani, imesababisha kufukuzwa kwake. 
    Kocha Carlos Dunga amefukuzwa kazi Brazil baada ya matokeo mabaya kwenye michuano ya Copa America Centenario inayoendelea nchini Marekani
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRAZIL YAMTUPIA VIRAGO KOCHA DUNGA SELECAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top