• HABARI MPYA

  Saturday, March 19, 2016

  RASMI, YANGA NA AHLY APRILI 9 DAR

  RASMI. Ni Yanga na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Hiyo inafuatia vigogo hao wa Misri kushinda 2-1 dhidi ya Recreativo do Libolo leo Uwanja wa Borg el Arab mjini Cairo katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza.
  Ahly iliyotoa sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza nchini Angola sasa itamenyana na wapinzani wao wa kihistoria kwenye michuano ya Afrika, Yanga mwezi ujao.

  Mara ya mwisho timu hizo zilikutana mwaka 2014 katika Raundi ya Kwanza na Yanga ikatolewa kwa penalti 4-3, baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake.
  Mechi ya kwanza itachezwa Aprili 9, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati marudiano yatakuwa Aprili 19 mjini Cairo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI, YANGA NA AHLY APRILI 9 DAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top