• HABARI MPYA

    Tuesday, February 21, 2012

    UHAMIAJI WAWATIA MATATANI MILOVAN, OKWI WAKIREJEA KUTOKA KIGALI

    KOCHA wa Simba, Cirkovic Milovan na mshambuliaji Emmanuel Okwi walijikuta kwenye wakati mgumu mbele ya maafisa uhamiaji wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere juzi.
    Maafisa uhamiaji hao waliwazuia Milovan na Okwi kwa zaidi ya dakika kumi kutokana na vibali vyao vya kufanya kazi nchini kuwa vya muda mfupi na pia siku zake za kumalizika zinakaribia.Kutokana na hali hiyo, viongozi wa Simba wakiongozwa na Katibu Evordus Mtawala waliingia kati na kuomba waruhusiwe kwani suala hilo linashughulikiwa kwa haraka.
    Akizungumza na gazeti hili baada ya kuruhusiwa, Milovan alisema kibali changu kimebakiza siku 15 na viongozi wanajua, lakini wanashindwa kulitatua."Kila siku na namueleza Mtawala suala hili, lakini yeye atakwambia kesho hadi sasa hajafanya hivyo si kitu kizuri kusumbuliwa hivi."
    "Nashindwa kufanya kazi vizuri, kutokana na usumbufu wa aina hii, nataka viongozi kesho (leo) waanze kufutilia jambo hili," alisema Milovan ambaye suala kibali chake pia lilikuwa tatizo kwenye uwanja wa ndege wa Kigali, Rwanda.
    Naye makamu mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu alisema ni kweli kibali cha kocha na wachezaji wao wa kigeni vilikuwa vimekatwa vya muda mfupi."Vibali vyao wote vimebakiza siku 15, lakini ni suala tutakalolishughulikia kwa haraka ili kuondoa usumbufu huu," alisema Kaburu.
    Naye katibu Mtawala alisema ni kweli kocha amekuwa akimkumbusha kila wakati kuhusu suala hilo.
    "Unajua kuna watu watano ambao tunapaswa kulipia vibali vyao na kibali kimoja dola 2000, watano dola 10,000 si fedha ndogo.
    "Tutalimaliza suala hili wiki hii kwa sababu siku 15 si nyingi tunaweza kupata usumbufu mwingine na watu wa uhamiaji," alisema Mtawala.
    Katika wachezaji watatu na makocha wawili waliosafiri na Simba kwenda Rwanda ni kiungo Partick Mafisango pekee aliyekuwa na kibali cha muda mrefu cha kufanya kazi nchini alichokatiwa na klabu ya Azam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UHAMIAJI WAWATIA MATATANI MILOVAN, OKWI WAKIREJEA KUTOKA KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top