• HABARI MPYA

    Tuesday, February 28, 2012

    REDONDO APATA TIMU MSUMBIJI, LAKINI...


    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Ramadhan Suleiman Chombo ‘Redondo’ amepata bonge la dini nchini Msumbiji, lakini tatizo anaiogopa klabu yake Azam, ataianzaje wakati aliitoroka kwenda huko.
    Redondo huyo wa Keko, amepata timu Msumbiji na hiyo si nyingine zaidi ya Ferroviarrio de Maputo, ambayo iko tayari kumpa mshahara wa dola 1,000 za Kimarekani kwa mwezi na dola nyingine za Kimarekani 9,000 kama dau la usajili.
    Hata hivyo, kitumbua cha mchezaji huyo kipo kwenye hatari ya kudondokea mchangani kutokana na masharti ya klabu hiyo, inayommiliki na kipa wa kimataifa nchini, Muharammi Mohamed ‘Shilton’.
    Ferroviarrio imemtaka Redondo kwanza awapatie hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ndipo akabidhiwe dola 9,000.
    Lakini kwa sababu Redondo aliondoka kwa kutoroka Azam FC, anaogopa ataanzaje kuzungumza na viongozi wake, hivyo amebaki Msumbiji tu anaangalia wenzake wanapocheza.
    Habari zaidi ambazo DIMBA imezipata zinasema kwamba, tayari Azam wamekwishashitukia dili hilo na wamesema hawatamuchia kiungo huyo hadi wapewe Sh. Milioni 35.
    Azam ilitaka kumtoa kwa mkopo Redondo kwenda Villa Squad Januari mwaka huu, lakini mchezaji huyo akagoma, lakini ajabu timu ilipoingia kambini hakuonekana tena hadi kuibuka habari yupo Msumbiji.
    Kiungo huyo wa zamani wa Simba na Ashanti, aliwahi pia kutakiwa na harasa El Hodooud ya Misiri mwaka juzi, lakini akaamua kuhamia Azam.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REDONDO APATA TIMU MSUMBIJI, LAKINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top