• HABARI MPYA

    Tuesday, February 28, 2012

    NIYONZIMA USO KWA USO NA YAKUBU KIGALI



    RWANDA, Amavubi wakiongozwa na Haruna Niyonzima wa Yanga, leo watakuwa wenyeji wa Nigeria, Super Eagles katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013. Huo utakuwa mchezo wa kwanza kati ya miwili baina ya timu hizo, ambao utachezwa kwenye Uwanja wa nyasi za bandia, mjini Nyamirambo, Kigali.
    Mara ya mwisho timu hizo zilikutana kwenye mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2006, mjini Kigali Juni, mwaka 2005, katika mchezo uliokwisha kwa sare ya 1-1. Nigeria ilishinda mchezo uliotangulia 2-0, Juni 2004.
    Chini ya kocha Milutin Sredojevic ‘Micho’, Amavubi ya Rwanda haijafungwa ndani ya mechi tano tangu Novemba 2011 wakati Super Eagles hawajafungwa katika mechi zao nne zilizopita tangu Oktoba 2011.
    Haya ni matunda ya soka inayofundishwa na kocha Stephen Keshi tangu aanze kuinoa Nigeria Novemba 2, mwaka 2011.
    Tangu Keshi achukue nafasi ya Ukocha Mkuu, Super Eagles haijafungwa ndani ya mechi tatu dhidi ya Botswana, Zambia na Liberia.
    Mtu mmoja hatari wa kuchungwa na Nigeria katika mchezo wa leo ni mshambuliaji wa APR FC, Oliver Karekezi.
    Katika Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa mjini Dar es Salaam, Tanzania, Desemba 2, Karekezi alipiga mabao matatu dhidi ya Djibouti katika michuano ya CECAFA Cup mwaka jana na kuiwezesha timu ya Micho kushinda 5-2.
    Siku sita baadaye alifunga tena katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwanda. Nigeria inatarajiwa kushuka uwanjani na mseto wa wachezaji wanaocheza nje na nchini mwao.
    Keshi anatarajiwa kutumia wachezaji wawili wanaocheza nyumbani katika safu ya ulinzi ambao watakuwa miongoni mwa Papa Idris, Godfrey Oboabona na Azubuike Egwuekwe.
    Mbele, Super Eagles inatarajiwa kubebwa na vipaji na uzoefu wa wakongwe, Yakubu Aiyegbeni na Peter Osaze Odemwingie, ambao kwa pamoja wana mabao 22 katika Ligi Kuu ya England msimu huu. Timu hiyo ya Magharibi mwa Afrika inaingia kwenye mchezo huo ikipewa nafasi kubwa ya kushinda, kwa sababu inashika nafasi ya nane katika viwango vya ubora wa soka Afrika vya FIFA wakati Rwanda ni ya 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIYONZIMA USO KWA USO NA YAKUBU KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top