• HABARI MPYA

    Saturday, February 25, 2012

    ADEBAYOR KILA KONA EMIRATES KESHO

    WAZOMEAJI, wapiga miluzi na waimbaji leo watakuwa na kazi moja ya kumshushia mvua ya kejeli mchezaji Emmanuel Adebayor, atakapokanyaga nyasi za Uwanja wa  Emirates akiwa na jezi za Tottenham Hotspur leo. Mashabiki wa Arsenal hawatapoteza muda kumuimba mshambuliaji wao wa zamani kuhusiana na ubinafsi wake na watamkumbusha tukio la basi lao la Togo lilivyopigwa risasi.
    Lakini klabu zote mbili zimekutana na na kumtaka Adebayor atulie kutokana na maneno machafu atakayotupiwa na mashabiki hao wa Emirates.
    Ni mchezo ambao utakaojawa na ushabiki mkubwa huku huku adui huyo namba moja wa Arsenal akitarajia kurushiwa maneno ya kebehi kutoka kwa mashabiki hao wa Gunners.
    Watakikumbuka kipindi ambacho nyota huyo aliondoka na kwenda kujiunga na Manchester City mwaka 2009 na vichwani mwa mashabiki wa Arsenal kutakuwa na kumbukumbu ya kitendo chake cha kufunga bao na kukimbia hadi kwa mashabiki wa Arsenal huku akisota na magoti kwenye nyasi na kushangilia.
    Ila pamoja na maneno na matusi watakayomrushia leo, Arsenal watapenda mchezaji huyo ajiunge kwenye kikosi hicho kutokana na kiwango alichokionyesha msimu huu.
    Adebayor, kwa sasa anakipiga katika klabu ya Spurs kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu na amekuwa kwenye kiwango kizuri akiwa na furaha, huku akiendelea kujikusanyia mashabiki kutoka kutokana na kazi anayoifanya kwenye kikosi cha Harry Redknapp.
    Tayari amepachika mabao 10 kwenye Ligi Kuu ya England na ametengeneza mabao 11 amekuwa kwenye kiwango kizuri tangua ameachwa kwenye kikosi cha City, ambapo alikuwa akigandishwa benchi kwenye kikosi cha Roberto Mancini.
    Kutokana na kiwango alichonacho Adebayor anaweza akawa kati ya wachezaji wagumu kuwadhibiti Ulaya, kasi yake, nguvu, akili na mawazo yake, anaweza akashika nafasi ya nne na ameonyesha kutoka na uwezo wake wa kumalizia mipira katika eneo la hatari.
    Kama atatulia, Adebayor atapata nafasi ya kicheko dhidi ya Arsenal iliyojeruhiwa katika mchezo huo wa timu  mahasimu wa Kaskazini mwa London, baada ya Gunners kuchapwa dhidi ya Milan na Sunderland.
    Je, leo ni njia gani itakuwa nzuri kwa Adebayor kufurahia miaka 28 yake ya kuzaliwa. Kwasasa Spurs iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, wakiwa na uhakika wa kufuzu Michuano ya Ligi ya Mabingwa na wako mbele kwa pointi 10 na majirani zao hao.
    Pengo hilo ni hatua kubwa kwa kwao, huku kikosi hicho cha Redknapp kikiwa na wachezaji wengi wenye vipaji kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji, dhidi ya Gunners ambao wamepoteza kujiamini wachezaji kama Adebayor, Gareth Bale na Luka Modric wataisumbua safu ya kikosi hicho cha Arsene Wenger wakitaka kupata ushindi wa pili ndani Emirates baada ya ule wa kwanza wakiwa White Hart Lane.
    Zikiwa zimesalia mechi 13 hadi kufikia mwisho wa msimu, Tottenham watakuwa wamemaliza ligi hiyo juu ya Arsenal kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995.
    Adebayor akiwa katika kiwango chake cha sasa ni ngumu kumdhibiti, aliwasili White Hart Lane akiwa na jina tokea Arsenal, lakini Spurs wamemfanya amekuwa tofauti.
    Tottenham watapenda kumbakisha kwenye kikosi hicho, lakini mshahara wake kwa wiki wa pauni 170,000 kwa wiki  inakuwa kazi kubwa kwa Spurs.
    Matusi kwa mashabiki ambao wanajua uwezo wake yatamfanya atake kuwaonyesha Gunners nini anaweza kufanya.
    Kama atafunga atataka kuwachokoza mashabiki wa Gunners, atafanya hivyo, lakini hatujui kitakachotokea kwa mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa anavaa jezi nyeupe za Spurs.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ADEBAYOR KILA KONA EMIRATES KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top