• HABARI MPYA

    Tuesday, February 21, 2012

    NIZAR AWAKOSA DRC

    WAKATI kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kiendelea na maandalizi ya mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ‘The Leopards’ utakaopigwa keshokutwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, Stars imepata pigo baada ya nyota wake wawili Juma Jabu na Stephano Mwasyika.
    Aidha, Stars katika mechi hiyo itawakosa nyota wake wawili wanaocheza nje ya nchi, Nizar Khalfan anayekipiga katika klabu ya Philadelphia Union ya Marekani na  Ally  Badru  Ally anayekipiga katika klabu ya  Canal Suez ya Misri.
    Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Stars kuelekea  mechi yake ya  mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbuji ambayo inatarajiwa kupigwa Februari 29 katika Uwanja huohuo.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema jana kwamba Juma Jabu ambaye aliumia na timu yake ya Simba ilipokuwa ikicheza na Kiyovu ya Rwanda katika mechi ya Shirikisho mwishoni mwa wiki, nafasi yake itachukuliwa na Waziri Salum wa Azam Fc, huku Mwasyika aliyeumia wakati akiitumikia timu yake ya Yanga ilipokwaana na Zamalek ya Misri katika ligi ya Mabingwa Afrika, hali yake inatarajiwa kuimarika ndani ya siku chache.
    Aliongeza kuwa Nizar na Badru hawatocheza mechi hiyo kutokana na kuchelewa kujiunga na kikosi cha Stars kwani kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la soka Afrika (CAF) mchezaji anatakiwa afanye mazoezi na timu yake ya Taifa kwa kipindi kisichopungua siku nne.
    Wambura alisema Stars kuwa kikosi cha Congo kinatarajiwa kuwasili jioni ya leo tayari kwa mchezo huo utakaorindima kuanzia saa 11 jioni.
    Kikosi cha Stars kinachonolewa na Mdenmark, Jan Poulsen kinaundwa na makipa Shabani Kado, Juma Kaseja na Mwadini Ali, huku mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa, Masoud Cholo, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Wazir Salum, Stephen Mwasika na Kelvin Yondani .
    Viungo  ni Jonas Gerald, Salum Abubakar , Jonas Gerard, Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe,  Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, na Abdi Kassim, huku washambuliaji ni Hussein Javu John Bocco, Nizar Khalfan, Mrisho Ngasa, Ally Badru Ally, Uhuru Selemani na Nsa Job.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    1 comments:

    Anonymous said... February 21, 2012 at 8:44 PM

    babu kubwa

    Item Reviewed: NIZAR AWAKOSA DRC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top