• HABARI MPYA

    Monday, August 05, 2019

    YANGA SC WAINGIA KAMBINI ZANZIBAR KUIKUSANYIA NGUVU TOWNSHIP ROLLERS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo asubuhi kwenda Zanzibar kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wake wa kwanza Raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana mwishoni mwa wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Hiyo ni baadaya jana kulazimisha sare ya 1-1 na Kariobangi Sharks ya Kenya katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kuhitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi. 
    Mechi ya marudiano itafanyika mjini Gaborone kati ya Agosti 23 na 25 na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Green Mamba ya Eswatini na Zesco ya Zambia.

    Kikosi kilichoingia kambini leo Yanga SC kinaundwa na makipa; Farouk Shikalo na Ramadhan Kabwili.
    Mabeki; Muharram Issa ‘Marcelo, Cleofas Sospeter, Ally Mtoni ‘Sonso’, Ally Hamad Ally na Lamine Moro.
    Viungo ni Mohamed Issa ‘Banka’, Raphael Daudi, Papy Kabamba Tshishimbi, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Mapinduzi Balama, Moustafa Suleiman, Gustafa Simon, Deus Kaseke na Mrisho Ngassa wakati washambuliaji ni Maybin Kalengo, Juma Balinya, Sadney Kholtage na David Molinga ‘Falcao’.
    Wachezaji wengine waliokuwa na timu ya taifa nchini Kenya kipa Metacha Mnata mabeki, Paul Godfrey, Kelvin Yondan na kiungo Feisal Salum watajiunga na timu kesho baada ya kurejea leo jioni kutoka Nairobi.
    Hata hivyo hakuna uhakika wa Yondan kwenda kambini, kwani yeye na Andrew Vincent ‘Dante’ na Juma Abdul waligoma kushinikiza wamalipwe stahiki zao. Kiungo Juma Shaaban Mahadhi yeye hayupo kambini kwa sababu ni majeruhi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAINGIA KAMBINI ZANZIBAR KUIKUSANYIA NGUVU TOWNSHIP ROLLERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top