• HABARI MPYA

    Tuesday, August 06, 2019

    WAZIRI MKUU, MAJALIWA NDIYE MGENI RASMI SIMBA DAY, WANACHAMA WAENDELEA KUCHANGIA DAMU

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, atakuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa kati ya klabu ya Simba na Power Dynamo kutoka nchini Zambia Jumanne jioni.                       
    Ofisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuwa katika mchezo wao huo utakaoanza saa 11, jioni mgeni rasmi ni Waziri Mkuu.
    Manara amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika ambapo kabla ya miamba hiyo ya soka kuvaana kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa hapa nchini.
    Amesema licha ya burudani hizi kutakuwa na mechi kadhaa za kirafiki pamoja na utambulisho wa wachezaji watakaocheza msimu Mpya, unaotarajia kuanza hivi karibuni.

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), atakuwa mgeni rasmi katika Simba Day Jumanne 

    "Maandalizi yamekamilika na mgeni rasmi ni Waziri Mkuu Majaliwa ambaye akuwepo na wanasimba kuadhimisha siku maalum ya Simba (Simba Day).
    Katika hatua nyingine, Tawi la klabu ya Simba, Never Give Up, limechangia damu, katika Hospitali Nguvu Kazi iliyopo Chanika Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya maazimisho ya wiki ya Simba (Simba Day).     
    Katika hafla hiyo iliyofanyika jana katika makao makuu ya Tawi hilo yaliyopo Masantula Chanika, ambapo wanachama na wapenzi wa Simba   walijitolea damu iliyopelekwa kwenye Hospitali hiyo.
    Katibu Mkuu wa tawi hilo Rashid Simba, amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutambua umuhimu wa jamii iliyowazunguka.
    Amesema katika tawi lao ambalo ni jipya walijipanga kujihusisha na mambo ya kijamii katika moja ya Hospitali zilizopo Ilala ambako ndiko lilipo tawi na makao makuu ya klabu yao.
    Aidha mwenyekiti wa Tawi hilo Hassan Njala amewashukuru wanasimba waliojitokeza katika uchangiaji huo.                  
    Naye mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dkt Kanansia Shoo, alipongeza Tawi hilo kwa kuchangia damu, kutokana na kuwa katika Wilaya hiyo tawi hilo ndiyo pekee lililofanya zoezi hilo.
    "Nawapongeza sana Wanasema wa Never Give Up kwa mchokifanya kwa sababu katika wilaya yetu ya Ilala ni ninyi pekee mlioweza kufanya hivi" Alisema Shoo.
    Leo Simba itakuwa katika tamasha maalum la wiki ya Simba (Simba Day) ambako kutakuwa na mchezo wa Kirafiki pamoja na kutambulisha wachezaji wa msimu Mpya wa Ligi Kuu  Tanzania Bara.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI MKUU, MAJALIWA NDIYE MGENI RASMI SIMBA DAY, WANACHAMA WAENDELEA KUCHANGIA DAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top