• HABARI MPYA

  Tuesday, August 06, 2019

  TANZANITE YACHAPWA 2-1 NA ZAMBIA COSAFA, KUMENYANA NA ZIMBABWE NUSU FAINALI

  Na Mwandishi Wetu, PORT ELIZABETH
  TIMU ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imepoteza mechi ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya kuchapwa 2-1 na Zambia jioni ya leo Uwanja wa Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
  Katika mchezo huo wa mwisho wa Kundi B, mabao ya Zambia leo yamefungwa na Florence Kasonde dakika ya nne na Christine Kalenge dakika ya 61, wakati la Tanzania lilifungwa na Enekia Kasonga dakika ya 84.
  Tanzania sasa itamenyana na Zimbabwe keshokutwa katika Nusu Fainali kuanzia Saa 5:00 asubuhi, wkaati Zambia itamenyana na wenyeji, Afrtika Kusini kuanzia Saa 9:00 Alasiri.  Pheromena Kizima wa Tanzania akijaribu kumtoka beki wa Zambia kwenye mchezo wa leo

  Leo Tanzania imepoteza mechi ya kwanza baada ya mwanzo mzuri, ikishinda mechi zake zote mbili za mwanzo 2-0 dhidi ya Botswana na 8-0 dhidi ya Eswatini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YACHAPWA 2-1 NA ZAMBIA COSAFA, KUMENYANA NA ZIMBABWE NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top