• HABARI MPYA

    Thursday, August 08, 2019

    SIMBA DAY ILIVYOFANA, ILIKUWA BURUDANI NJE NA NDANI TAIFA

    Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
    Ilikuwa bomba sana ninaweza kusema mashabiki wa Simba wamefanikiwa kuibadili siku ya kazi kuwa wikendi na kuifanya Jumanne kuwa sikukuu,mji ulizizima,siwezi kuandika sana bila kusema hili maana nisije kusahau Haji Manara unastahili hongera maalumu uwezo wako wa kuhamasisha na kutengeneza mvuto wa jambo ni kitu ambacho mungu amekupa hongera brother endelea kutumia uwezo wako maana mungu alikujalia kwa sababu leo na kesho uwenda wapo ambao hawajaona ila ipo siku watakuelewa. Siku za karibuni sijaona mtaalamu wa propaganda aliyefanikiwa zaidi yako brother hongera tumeona,tumekubali.
    Kwa ujumla wake nitoe pongezi kwa uongozi wa Simba sc kwani mmeendelea kushikana na kupigania kile mnachokiamini na hajakubali kugawanywa na kweli Siku ya jana mmethibitisha kwa tukio kubwa lenye mvuto wa Aina yake katika historia ya soka letu Asanteni sana..
    Nimeanza kwa kusema ilikuwa burudani nje ndani nikimaanisha haya.

    NJE.
    Umati ulikubali mwitikio mkubwa,rangi nyekundu zilitawala viunga vyote vya uwanja wa Taifa shangwe kubwa,nderemo ,vifijo na bashasha kila mahali mashabiki walijitoa hasa,waliacha shughuli zao kuja kuifuata timu yao hawakujali chochote zaidi ya kuanikiza mda wote mbele ya mashujaa wao walionesha thamani halisi ya simba siku ya jana. Hapa ndipo unaweza kuona thamani za mchezo wa soka nina imani katika nchi nyingi za Afrika hata mabara mengine ni nadra kuona mambo kama haya ila Tanzania yapo na miongoni mwao ni Simba SC hivyo mashabiki walitoa burudani ya kutosha na kupendezesha siku hiyo maalumu kwa klabu ya Simba.

    NDANI.
    Kikubwa kilichosababisha siku ya jana ni uwepo wa kikosi cha Simba ambacho kilianza kwa kutambulishwa kwa mashabiki na wapenzi wa soka na kisha kukata mzizi wa fitna kwa mchezo wa kirariki wa kimataifa dhidi ya klabu ya Power dynamo kutoka Zambia mchezo ambao ullikuwa mzuri na wa kuvutia huku Dynamo wakizidiwa maeneo yote na kupagaishwa na shangwe za kutosha kutoka mashabiki na wapenzi wa Simba nina imani wataenda kusimulia walichokiona uwanja wa Taifa.

    TATHIMINI FUPI.
    Simba walianza kwa spidi sana mchezo wa jana wakitumia mfumo wa 4-3-3 wakiwa na walinzi 4 ambao waliongozwa vema na Pascal Wawa ambaye alicheza vizuri na mbrazili Santos da Silva huku walinzi wa pembeni Kapombe na Mohamed Husein wakitumika vema katika kupeleka mashambulizi kupitia pembeni wakitumika kama wingback.
    Sehemu ya kiungo ilikuwa na viungo watatu ambao katikati yao alisimama vema Shaibob ambaye ni mzuri kwenye umiliki wa mpira na ni miongoni mwa viungo wabunifu akisaidiwa na Mzamiru Yasini na Chama ambao waliutanua uwanja na kuwapisha kapombe na mohamed husein kupita ili kwenya kumimina majalo kwa safu ya ushambuliaji ambayo iliongozwa vema na Meddie Kagere akiwa mshambuliaji wa kati huku akisaidiwa na Fransis Kahata na Deo Kanda ambaye ni machachari sana katika kuuchezea mpira.
    Kwa matumizi ya mfumo wa 4-3-3 na kikosi kilicho anza naweza sema walifanikiwa kwa asilimia 65 kwani walikuwa wazuri sana walipo miliki mpira na kuonesha uchangamfu zaidi katika eneo la kiungo ingawa pindi walipo poteza mpira walikuwa wazito kukaba na kuna wakati walionekana kutembea katika eneo la kati kitu ambacho ni hatari pindi utakapokutana na timu inayotumia vema mashambulizi ya kushitukiza.
    Kazi inayofanywa na Kapombe na Tshabalala ni nzuri sana ila inatakiwa  kuwe na uharaka wa kurudi endapo wanapoteza mpira kwani viungo ambao ndio wanakuwa nyuma yao pindi wao wanapoenda kushambulia sio wazuri sana wa kukaba pia hawana spidi jambo linaloweza kuleta matatizo hasa kwenye maeneo  ya pembeni pale utakapokutana na timu yenye winga wazuri na wenye mbio pia.
    Eneo la ushambuliaji ameonekana Meddie Kagere akiwa mbali sana zaidi ya wasaidizi wake na bado hakupata mtu wa kuendana naye kwa kikosi cha jana nazidi kuona muunganiko wake na John Bocco ukiendelea kushamili kwani sikuona mipango ikipangwa kati ya Deo Kanda,kahata na Kagere  kitu ambacho kitapunguza nguvu endapo timu pinzani itafanikiwa kumdhibiti meddie kagere,sikushangaa kuona magori yote matatu akifunga kwa kuyatafuta yeye mwenyewe hivyo benchi la ufundi kuna haja ya kufanya kitu katika safu ya ushambuliaji.
    Jambo jingine bado spidi sio kubwa pindi timu inapokuwa na mpira na kuanza kutengeneza mashambulizi kuelekea mbele kitu kinachopelekea timu pinzani kurudi na kuziba mianya na kupelekea ugumu katika kushambulia.
    Yote kwa yote timu ni nzuri,pana lakini pia wachezaji wa kigeni waliosajiliwa wanatakiwa kuongeza kasi ili kuendana na kasi ya simba lakini pia Deo Kanda anatakiwa kucheza kwa kuleta madhara kwa timu pinzani hasa timu ikiwa inasaka ushindi.
    Na endapo 4-3-3 ndio utakuwa mfumo mama wa timu ni vema kuhakikisha wachezaji wanakuwa na kasi mda wote wa mchezo ni mfumo unaotaka kushambulia kama timu na kukaba kama timu pia uku safu ya ulinzi ikipunguza makosa ya mipira ya krosi na kona tatizo ambalo limekuwa la mda sasa...
    Mwisho viongozi na wanachama hongereni sana kwa kazi nzuri huu ni mwanzo mwema kikubwa ni kuhakikisha mnaendeleza moto huu mliouwasha siku ya jana.
    Ahsanteni.

    (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka,pia anapatikana katika Instagram akaunti yake kupitia@dominicksalamba +255713942770)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA DAY ILIVYOFANA, ILIKUWA BURUDANI NJE NA NDANI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top