• HABARI MPYA

  Thursday, August 08, 2019

  TANZANIA YAWAPIGA AFRIKA KUSINI 2-0 NA KUTINGA FAINALI COSAFA U20 WANAWAKE

  Na Mwandishi Wetu, PORT ELIZABETH
  TIMU ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Afrika Kusini jioni ya leo Uwanja wa Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth.
  Mabao ya Tanzanite katika mchezo wa leo yamefungwa na Enekia Kasonga dakika ya 18 na Opa Clement Sanga dakika ya 30. 
  Baada ya mchezo huo, mchezaji wa Tanzanite, Enekia Kasongo alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi, timu hiyo ikiendelea kutoa mchezaji wa mechi zote ilizocheza.

  Opa Sanga ameifungia Tanzanite bao la pili leo ikiilaza Afrika Kusini 2-0


  Sasa Tanzanite itakutana na Zambia katika fainali Jumapili, ambayo imeitoa Zimbabwe kwa kuichapa 1-0, bao pekee la Mary Mambwe dakika ya 32.
  Huo utakuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo, baada ya Zambia kuichapa Tanzajia 2-1 kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B.
  Siku hiyo, mabao ya Zambia yalifungwa na Florence Kasonde dakika ya nne na Christine Kalenge dakika ya 61, wakati la Tanzania lilifungwa na Enekia Kasonga dakika ya 84.
  Mechi nyingine za Kundi B, Tanzania ilishinda mechi zake zote mbili 2-0 dhidi ya Botswana na 8-0 dhidi ya Eswatini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAWAPIGA AFRIKA KUSINI 2-0 NA KUTINGA FAINALI COSAFA U20 WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top