• HABARI MPYA

    Saturday, August 10, 2019

    PAMBANO LA MARUDIANO RUIZ NA JOSHUA DESEMBA 7 SAUDI ARABIA

    PAMBANO la marudiano kati ya Anthony Joshua na Andy Ruiz Jr litafanyika Deaemba 7 mjini Diriyah nchini Saudi Arabia. 
    Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo, imethibitisha pambano hilo la kuwania mataji ya IBF, WBA na WBO litafanyika Uarabuni mwishoni mwa mwaka.
    Jiji la New York na Uwanja wa Cardiff waliwania kuwa wenyeji wa pambano hilo, lakini wakazidiwa kete na Diriyah kufuatia Mamlaka ya Michezo ya Saudi Arabia kuweka kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 100 kupewa uenyeji. 

    Pambano la marudiano Anthony Joshua na Andy Ruiz Jr litafanyika Deaemba 7 mjini Diriyah nchini Saudi Arabia PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    AJ anatarajiwa kuzichapa tena na Mmexico baada ya kuchapwa kwenye pambano la kwanza ukumbi wa Madison Square Garden, New York nchini Marekani Juni 1, mwaka huu.
    Joshua mwenye urefu wa futi sita alivuliwa mataji yake yote ya dunia ya uzito ya IBF, WBA na WBO baada ya kupigwa na Ruiz kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba.
    Hilo lilikuwa ni pambano la kwanza Joshua kupoteza baada ya kushinda mapambano yake yote 22 ya awali, 21 kwa knockout, wakati Ruiz mwenye urefu wa futi nne alishinda pambalo la 32 na 22 kwa KO, huku akiwa amepoteza pambano moja pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBANO LA MARUDIANO RUIZ NA JOSHUA DESEMBA 7 SAUDI ARABIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top