• HABARI MPYA

  Saturday, August 10, 2019

  KMC YATOA SARE O-0 NA AS KIGALI RWANDA, KMKM YACHAPWA 2-0 NA AGOSTO ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  TIMU ya KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam leo imelazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, AS Kigali katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda.
  Ikiongozwa na kipa mkongwe, Juma Kaseja aliyeiongoza Tanzania kuitoa Kenya katika kinyang'anyiro cha tiketi ya CHAN ya mwakani Cameroon, KMC iliibana sawia AS Kigali nyumbani leo.
  Sasa KMC inayofundishwa na kocha Mganda, Jackson Mayanja itakuwa na shughuli nyepesi kidogo kwenye mchezo wa marudiano nyumbani, Dar es Salaam wiki ijayo ikitakiwa kushinda ili kusonga mbele.

  Juma Kaseja ameisaidia KMC kupata sare ya ugenini dhidi ya AS Kigali mjini Kigali leo Kombe la Shirikisho 

  Ikumbukwe mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Proline FC ya Uganda anapotokea kocha wao, Jackson Mayanja na Masters Security Services ya Malawi.
  Nao wawakilishi wa Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa, Malindi SC wamechapwa 2-0 na na Primiero de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabao ya Primiero de Agosto leo yamefungwa na Lionel Yomb dakika ya tisa na Manuel David dakika ya dk 71 na mchezo wa marudiano utafanyika wiki ijayo mjini Lunada wakati mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Green Eagles FC ya Zambia na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YATOA SARE O-0 NA AS KIGALI RWANDA, KMKM YACHAPWA 2-0 NA AGOSTO ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top