• HABARI MPYA

  Thursday, August 16, 2018

  SAMATTA AFUNGA BAO MUHIMU UGENINI GENK YABISHA HODI MAKUNDI EUROPA LEAGUE

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku huu ameifungia timu yake, KRC Genk bao la kwanza ikishinda 2-1 ugenini dhidi ya Lech Poznan ya Poland kwenye mchezo wa marudiano Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya UEFA Europa League Uwanja wa INEA mjini Poznan.
  Kwa matokeo hayo, KRC Genk inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita, Samatta pia akifunga bao moja.
  Genk sasa wanafuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi, ambako watacheza mechi moja zaidi nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ataingia hatua hiyo.

  Mbwana Samatta (kushoto) akishangilia na mchezaji mwenzake baada ya kufunga leo Uwanja wa INEA mjini Poznan

  Samatta aliyefunga bao la pili kwenye mechi ya kwanza mjini Genk dakika ya 56, baada ya kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy kutangulia kufunga la kwanza dakika ya 44 – leo alifunga la kwanza dakika ya 19 tu.
  Bao la pili la Genk limefungwa na Leandro Trossard kwa penalti dakika ya 45, wakati la wenyeji limefungwa na Tomasz Cywka dakika ya 50.    
  Samatta aliyejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya DRC, ambayo nayo ilimtoa Simba SC ya nyumbani, Tanzania mwaka 2011 anawindwa na klabu kadhaa za Borussia Dortmund ya Ujerumani, Levante ya Hispania na CSKA Moscow ya Urusi.
  Kikosi cha KKS Lech Poznan kilikuwa; Buric, De Marco, Rogne/Orlowski dk28, Gajos/Jevtic dk72, Cywka, Kostevych, Amaral, Tiba, Janicki, Jozwiak na Gytkjaer/Tomczyk dk72.
  KRC Genk : Vukovic, Uronen, Dewaest, Aidoo, Maehle, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Piotrowski dk60, Trossard/Zhegrova dk60, Samatta na Ndongala.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA BAO MUHIMU UGENINI GENK YABISHA HODI MAKUNDI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top