• HABARI MPYA

    Tuesday, August 14, 2018

    MADAKTARI WAWILI WANUFAIKA NA NYUMBA ILIYOMALIZIWA NA SPORTPESA MBELE YA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA

    Kizimkazi, ZANZIBAR
    MKURUGENZI wa Utawala Na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas amehudhuria shighuli ya ukaguzi wa miradi mbali mbali ikiwemo Nyumba ya kuishi madaktari wawili wa zahanati ya Kizimkazi Wilaya Ya Kusini Unguja, Zanzibar linalofadhiliwa na kampuni ya SportPesa ambapo Jengo Hilo limezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan.
    Akizingumza kwenye hafla ya Uzinduzi wa Jengo Hilo Tarimba Alisema anawashukuru wananchi wa Kizimkazi kwa kuwaamini na kuona Kuwa Sportpesa inaweza kuwasaidia na kuamua kurudisha fadhila kwa jamii.
    "Mara zote tumekuwa tunashirikiana na Jamiii Na Ndio Maana Baada ya Kuombwa Kufadhili Ujenzi wa Nyumba ya Kuishi Daktari wa Zahanati ya Kizimkazi hatukusita kukubaliana na ombi lenu"





    Mkurugenzi Huyo Kutoka Sportpesa alisema walipotembelea Jengo Hilo Kabla ya kuanza rasmi ukarabati mnamo mwezi Februari halikuwa Katika muonekano mzuri na salama Kwa Daktari anayehudumia Afya za wananchi wa eneo hilo kuishi.
    Aidha Tarimba Amewataka Madaktari watakaoutumia Nyumba hiyo kuhakikisha wanaitunza vizuri kwani hiyo itasaidia jengo kudumu kwa muda mrefu na kuwa msaada kwao na wananchi kwa ujumla
    Kwa upande wa Daktari wa zahanati ya Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja Bi Suleha Nuhuu ambaye ndiye ataitumia nyumba hiyo kama makazi ameshukuru uongozi wa SportPesa kwa kukamilisha umalizikaji wa jengo hilo na kwa juhudi walizozionyesha kwa kukamilisha jengo wa wakati.
    "Tunaishukuru sana SportPesa kweli walikuja na tulipowaomba watusaidie wakakubali kwangu kama daktari imekuwa rahisi maana sitokaa mbali tena na zahanati hii",alisema Nuhuu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MADAKTARI WAWILI WANUFAIKA NA NYUMBA ILIYOMALIZIWA NA SPORTPESA MBELE YA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top