• HABARI MPYA

    Tuesday, August 14, 2018

    BAADA YA KUFUNGWA MABAO 35 KATIKA MECHI 44 YOUTHE ROSTAND HAFAI YANGA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    JULAI 29, mwaka huu mlinda mlango Mcameroon, Youthe Juhe Rostand aliidakia kwa mara ya mwisho klabu ya Yanga SC ikipoteza mchezo wa tatu katika Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kufungwa 3-2 na Gor Mahia ya Kenya.
    Baada ya mchezo huo, uongozi ulikutana naye kwa majadiliano ya kuvunja mkataba ambayo hatimaye yalizaa makubaliano ya kiungwana, kuachana salama.
    Sababu za uongozi wa Yanga kuamua kuvunja mkataba na Rostand ni kelele za mashabiki ambao hawakuridhishwa na udakaji wake kutokana na kuruhusu mabao rahisi mara nyingi.
    Na baada ya kufungwa mabao mengine rahisi Julai 29, mashabiki wakiondoka uwanjani wanasononeka kwa kipigo cha nyumbani, uongozi ukaona suluhisho ni kumruhusu kuondoka.

    Kipa Mcameroon, Youthe Juhe Rostand ameachwa Yanga SC baada ya msimu mmoja tu 

    Youthe amedumu Yanga kwa msimu mmoja tu baada ya kusajiliwa Julai mwaka jana kutoka African Lyon ya Dar es Salaam iliyoshuka Daraja.
    Alisajiliwa Yanga SC baada ya kuwavutia mashabiki na viongozi walipomuona akidaka vizuri na kuwapa wakati mgumu mahasimu, Simba SC msimu wa 2016-2017.
    Na Yanga SC hawakutaka kujua kwa nini African Lyon inateremka Daraja baada ya msimu wa 2016-2017, wakaangalia tu namna Rostand alivyodaka katika mechi kubwa dhidi ya wao wenyewe, (Yanga), Azam FC na Simba.
    Hatimaye baada ya mechi 44, akifungwa mabao 35, ukiondoa yale ya penalti za baada ya matokeo ya sare kwenye mechi za mtoano, historia ya Youthe Jehu Rostand inafungwa Yanga SC.  
    Mechi yake ya kwanza kudaka ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Singida United Agosti 5, mwaka jana Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam akiruhusu mabao mawili, Yanga ikishinda 3-2.
    Akadaka vizuri bila kuruhusu bao ndani ya dakika 90 kwenye mechi ya kuwania Ngao ya Jamii Agosti 23, mwaka jana Uwanja wa Taifa, lakini Yanga ikaenda kufungwa kwa penalti 5-4.
    Tangu hapo, Rostand akawa ni kipa asiyetabirika wakati fulani akidaka vizuri na wakati mwingine akifungwa kwa urahisi mno na haikuwa ajabu matokeo ya klabu yakawa yasiyofurahisha pia.
    Na kutokana na ukweli kwamba hali ya kifedha ya klabu msimu uliopita haikuwa nzuri, morali ya wachezaji nayo ikazidi kushuka hali ambayo ilisababisha wachezaji wengi kucheza chini ya uwezo wao.
    Wachezaji wa Yanga katika mechi za karibuni wamekuwa hawajitumi kabisa, lakini Rostand akajikuta anabeba lawama zaidi kwa sababu tu ndiye mlinda mlango, sehemu ambako mabao yanapitia. Na ni kweli, kufungwa mabao 35 katika mechi 44 ni takwimu zisizopendeza na huyo hawezi kipa namba moja wa klabu.

    MATOKEO YA MECHI ZOTE ALIZODAKA YOUTHE ROSTAND YANGA SC NA MABAO ALIYOFUNGWA
    Yanga 3-2 Singida United (Hakufungwa, aliingia kipindi cha pili akaokoa penalti)
    Yanga 1-0 Chipukizi (Alianza kipindi cha kwanza tu kirafiki Zanzibar)
    Yanga 0-0 (4-5 penalti) Simba (Alifungwa penalty tano Ngao ya Jamii, Taifa)
    Yanga 1 – 1 Lipuli (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 1-0 Njombe Mji (Hakufungwa Ligi Kuu Saba Saba, Njombe)
    Yanga 1-1 Maji Maji (Alifungwa moja Ligi Kuu Maji Maji, Songea)
    Yanga 1-0 Ndanda (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 0-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 2-1 Kagera Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Bukoba)
    Yanga SC 4-0 Stand United (Hakufungwa Ligi Kuu Kambarage, Shinyanga)
    Yanga 1-1 Simba (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 0-0 Singida United (Hakufungwa Ligi Kuu Namfua, Singida)
    Yanga 5-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 1-1 Tanzania Prisons (Alifungwa moja, Ligi Kuu Chamazi)
    Yanga SC 2-0 Reha FC (Hakufungwa 64 Bora Kombe la TFF Uhuru)
    Yanga SC 0-2 Mbao FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kirumba)
    Yanga SC 1-0 JKU (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 1-1 Singida United (Alifungwa moja Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga SC 0-0 (pen4-5) URA (Hakufungwa Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
    Yanga 0-0 Mwadui FCi (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 1-0 Ruvu Shooting  (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
    Yanga 2-1 Azam FC  (Alifungwa moja Ligi Kuu Chamazi)
    Yanga 1-1 (pen4-3) Ihefu FC  (Alifungwa moja, akaokoa penalti tatu Kombe la TFF Sokoine, Mbeya)
    Yanga 2-0 Lipuli FC  (Hakufungwa, alitoka dk17 baada ya kuumia, Samora, Iringa)
    Yanga 1-1 Saint Louis FC  (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa, Mahe)
    Yanga 2-1 Maji Maji FC  (Alifungwa moja Kombe la TFF Maji Maji, Songea)
    Yanga 2-1 Ndanda FC  (Alifungwa moja Ligi Kuu, Nangwanda)
    Yanga 3-0 Kagera Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu, Taifa)
    Yanga 3-1 Stand United (Alifungwa moja Ligi Kuu, Taifa)
    Yanga 0-0 Township Rollers  (Ligi ya Mabingwa Gaborone)
    Yanga 1-1 (Penalti 2-4) Singida United (Alifungwa moja na penalty nne Kombe la TFF Maji Maji, Namfua)
    Yanga 2-0 Wolaita Ditcha  (Hakufungwa Kombe la Shirikisho Dar es Salaam)
    Yanga SC 1-1 Singida United (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 0-1 Wolaita Ditcha  (Alifungwa moja Kombe la Shirikisho Hawassa)
    Yanga 1-1 Mbeya City (Alifungwa moja Ligi Kuu, Sokoine)
    Yanga SC 0-1 Simba (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
    Yanga SC 0-4 U.S.M. Alger (Alifungwa nne, moja la penalti Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika)
    Yanga 0-4 U.S.M. Alger   (Alifungwa nne Kombe la Shirikisho Algiers)
    Yanga 0-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Jamhuri)
    Yanga SC 0-0 Rayon Sport (Hakufungwa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Taifa)
    Yanga 0-1 Mwadui FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Kambarage)
    Yanga 1-0 Mbao FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
    Yanga 1-3 Kakamega Homeboyz FC (Alifungwa tatu SportPesa Super Cup Nakuru)
    Yanga SC 2-3 Gor Mahia (Alifungwa tatu Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Taifa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAADA YA KUFUNGWA MABAO 35 KATIKA MECHI 44 YOUTHE ROSTAND HAFAI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top