• HABARI MPYA

  Friday, March 02, 2018

  NEYMAR SASA HATARINI KUKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA

  MSHAMBULIAJI Neymar amewasili nchini Brazil jana akiwa kwenye kiti cha walemavu kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake — huku nyota huyo wa Paris Saint-Germain akiwa hatarini kutocheza fainali za Kombe la Dunia katikati ya mwaka nchini Urusi. 
  Mbrazil huyo alihitaji msaada wa wasaidizi wa Uwanja wa Ndege wakat anawasili mjini Rio de Janeiro na kifundo chake cha mguu wa kulia kilionekana kimefungwa wakati anasukumwa eneo la Uwanja wa Ndege.
  Neymar mara moja atasafiri kwenda Belo Horizonte, ambako ndiko atafanyiwa upasuaji wa maumivu yake aliyoyapata Jumamosi iliyopita.  

  Neymar yuko hatarini kutocheza fainali za Kombe la Dunia katikati ya mwaka nchini Urusi PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  RATIBA YA BRAZIL KOMBE LA DUNIA 

  Jumapili Juni 17: 
  v Uswisi
  Ijumaa Juni 22: 
  Costa Rica
  Jumatano Juni 27: 
  Serbia 
  Amevunjika mfupa wa kifundo chake cha mguu katika mechi ya Jumapili timu yake, PSG ikishinda 3-0 dhidi ya Marseille. 
  Awali PSG walidhani hayatakuwa maumivu makubwa, lakini nyota wao sasa anaelekea kukosa sehemu yote ya msimu iliyobaki hadi Fainali za Kombe la Dunia, Urusi. 
  Kwa mujibu wa Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa hadi miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji.
  Rodrigo Lasmar, amenukuliwa na tovuti ya gazeti la O Globo la Brazil akiseam kwamba mchezaji huyo ghali zaidi duniani atakuwa nje kwa muda mrefu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR SASA HATARINI KUKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top