• HABARI MPYA

  Friday, March 02, 2018

  KANE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA LONDON

  MSHAMBULIAJI Harry Kane amekuwa mshindi wa tuzo za Wanasoka London kwa kupewa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka.
  Nyota huyo wa Tottenham amefanya vizuri kwa miezi 12 iliyopita na ilikuwa sahihi kupewa tuzo hiyo.
  Amewashinda Cesar Azpilicueta, wachezaji wenzake Heung-Min Son na Christian Eriksen, na Wilfried Zaha.
  Kocha wa Crystal Palace, Roy Hodgson amebeba tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Battersea Evolution.
  Kocha huyo wa zamani wa England amepewa heshima hiyo mbele ya akina Mauricio Pochettino na Slavisa Jokanovic.
  Kinda mwenye kipaji, Ryan Sessegnon ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka.

  Harry Kane ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka katika tuzo za Wanasoka London PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mchezaji huyo mwenye umei wa miaka 17 wa Fulham amekuwa na msimu mzuri kiais cha kuwavutia wapinzani, Spurs ya London pia.
  Sessegnon, ambaye alikabidhiwa tuzo yake na Bobby Zamora, pia alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
  Daniel Bentley wa Brentford ameshinda tuzo ya Kipa Bora wa Mwaka akiwazidi Thibaut Courtois na Hugo Lloris.
  Mechi baina ya QPR na Grenfell kuchangisha fedha kwa ajili ya waathirika wa janga la moto mwaka jana, imepewa tuzo ya Mradi Bora wa Maendeleo ya Jamii wa mwaka.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KANE ASHINDA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top