• HABARI MPYA

  Thursday, March 01, 2018

  LUKAKU ASAINI MKATABA WA KUMILIKIWA NA KAMPUNI YA JAY Z

  MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku amejiunga na kampuni ya umiliki wanamichezo ya gwiji wa Hip hop, Jay-Z iiitwayo Roc Nation Sports.
  Mchezaji huyo wa Manchester United ameposti picha tatu kwenye ukurasa wake wa Instagram na akisema; 'ukaribisho kwenye familia' mjini New York. 
  Kampuni ya  Roc Nation ya Jay-Z ilianza kujipatia umaarufu katika katika kuibua vipaji vya wasanii na sasa inavuka mipaka kwa ujio wa Roc Nation Sports na Lukaku anakuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu ya England kusainiwa. 

  Romelu Lukaku amejiunga na kampuni ya Roc Nation Sports inayomilikiwa na Rapa, Jay Z PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  ROC NATION SPORTS 

  Roc Nation Sports ni idara ya kumiliki wanamichezo katika Roc Nation, kampuni ya sanaa iliyoanzishwa na Jay-Z.
  Tawi la Michezo lilianzishwa mwaka 2013 kwa lengo la kuwasaidia wanamichezo na kuwaendeleza ndani na nje ya Uwanja. 
  Mikataba ya kibiashara, mahusiano na vyombo vya Habari na kumkuza mchezaji kuwa bidhaa kubwa yote ni mambo ambayo Roc Nation Sports huwafanyia wateja wake. 
  Wateja maarufu ni: 
  Kevin Durant, Dez Bryant, Jerome Boateng, Miguel Cotto, Romelu Lukaku 
  Mbelgiji huyo anakuwa mwanasoka wa pili baada ya beki wa Bayern Munich, Jerome Boateng kujiunga na kampuni hicho. 
  Zaidi kampuni ya Roc Nation Sports inamiliki wanamichezo wa boasts a clientele from the NFL, MLB na NBA na majina mengine makubwa waliompokea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. 
  Jacksonville Jaguars alimzunguka Leonard Fournette kubadilishana jezi na Lukaku.
  Mshambuliaji huyo pia alipiga picha na wakali wengine wa Marekani, Victor Cruz na Shawn 'Pecas' Costner, Ofisa mkubwa wa wa Roc Nation Sports.
  Hakuna shaka kusainiwa kwa Lukaku ni hatua nzuri kwa kampuni hiyo na walifanuya sherehe ya kuwakaribisha katika zulia jekundu. 
  Costner aliandika kwenye Instagram yake: "Wanafamilia wakimkaribisha Romelu Lukaku familia ya Roc Nation Sports.'
  Na Lukaku akatumia muda wake wa mapumziko baada ya ruhusa aliyopewa Man United kwenda kutazama mechi ya Brooklyn Nets akiwa ameketi kwenye viti vya pembezoni mwa Uwanja.
  Mshambuliaji huyo atarejea Manchester akiwa na ari mpya, kwa ujumla baada ya kutoa mchango mkubwa katika ushindi wa 2-1 dhidi ya timu yake zamani, Chelsea kwa kufunga bao la kusawazisha na kuseti la ushindi. 
  Kwa kuchanganya na furaha ya kusainiwa Roc Nation Sports, anatarajiwa kuendeleza makali yake katika mechi ijayo dhidi ya Crystal Palace Jumatatu usiku.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU ASAINI MKATABA WA KUMILIKIWA NA KAMPUNI YA JAY Z Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top