• HABARI MPYA

  Friday, March 02, 2018

  YANGA SC WAINGIA KAMBINI LEO KUANZA KUJIPANGA KWA AJILI YA TOWNSHIP ROLLERS

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga imerejea jana jioni mjini Dar es Salaam kutoka Mtwara na leo inaingia kambini kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana wiki ijayo.
  Yanga SC juzi ilipata ushindi wake wa kwanza Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara dhidi ya wenyeji, Ndanda FC tangu mwaka 2015 baada ya kuwachapa 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom. Tanzania Bara.
  Na baada ya ushindi huo unaoweka hai matumaini ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu, Yanga ya kocha George Lwandamina anayesaidiwa na Mzambia mwenzake, Noel Mwandila na wazalendo, Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali kocha wa makipa inahamishia mawindo yake kwenye michuano ya Afrika.
  Yanga inaingia kambini leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Township Rollers ya Botswana Jumanne 

  Yanga watakuwa wenyeji wa Township Rollers ya Botswana Jumanne katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa, kabla ya timu hizo kurudiana siku 10 baadaye Gaborone.
  Kuelekea mchezo huo habari njema ni kwamba, viungo washambuliaji, mzawa Juma Mahadhi aliyekuwa anasumbuliwa na homa, Mzimbabwe Thabani Kamusoko majeruhi wa muda mrefu, Mzambia Obrey Chirwa aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya misuli wote wamepona.      
  Na wote wanatarajiwa kuingia kambini leo katika siku nne nzito za kujiandaa kwa vita ya kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAINGIA KAMBINI LEO KUANZA KUJIPANGA KWA AJILI YA TOWNSHIP ROLLERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top