• HABARI MPYA

  Sunday, May 21, 2017

  MASIKINI WENGER, PAMOJA NA USHINDI ARSENAL YAIKOSA LIGI YA MABINGWA

  Arsene Wenger akiwa amejiinamia Uwanja wa Emirates leo licha ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England, kwa sababu haijamsaidia kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya tano, nyuma ya Liverpool, nafasi ya nne, Manchester City ya tatu, Tottenham Hotspur ya pili na Chelsea waliotwaa ubingwa. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Hector Bellerin dakika ya nane, Alexis Sanchez dakika ya 27 na Aaron Ramsey dakika ya 90 na ushei, wakati la Everton limefungwa na Romelu Lukaku dakika ya 58 kwa penalti. Laurent Koscielny alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 14 baada ya kumchezea rafu Enner Valencia na atakosa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASIKINI WENGER, PAMOJA NA USHINDI ARSENAL YAIKOSA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top