• HABARI MPYA

  Saturday, October 01, 2016

  YANGA B WAWASAFISHIA KAKA ZAO, WAWATANDIKA SIMBA B 2-0 TAIFA

  TIMU ya vijana ya Yanga chini ya umri wa miaka 20, imeifunga Simba B mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa utangulizi kabla ya mechi baina ya timu za wakubwa za klabu hizo mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Shukraan kwao, wafungaji wa mabao hayo Ayoub M Ayoub dakika ya 16 na Paul Godfrey dakika ya 38 ambao wamewafanya mashabiki wa Yanga waanze kushangilia mapema.
  Kiungo wa Simba B, Dadi Mbarouk (katikati) akikimbia na mpira dhidi ya wachezaji wa Yanga B, Ally Mbondele (kushoto) na Maka Edward (kulia) 
  Paul Godfrey (katikati) akishangilia baada ya kufunga bao la pili

  Yanga B, inayofundishwa na beki wake wa zamani, Nsajigwa Shadrack Mwandemele leo iliwazidi kabisa wapinzani wao walio chini ya kocha Nico Kiondo, kiungo wa zamani wa Simba.   
  Mchezo baina ya vikosi vya kwanza vya Simba na Yanga wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unafuatia Saa 10:00 jioni ya leo uwanjani hapo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA B WAWASAFISHIA KAKA ZAO, WAWATANDIKA SIMBA B 2-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top